Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United, Tottenham kazi ipo

Muktasari:

  • Wikiendi hii mechi za Ligi Kuu zinapumzika na kinachoenda kufanyika ni mtifuano wa raundi ya nne ya Kombe la FA na klabu zinawania taji hilo ambalo lina faida kwenye michuano ya kimataifa.

LONDON, ENGLAND: ZINAJITAFUTA. Ndiyo, miamba miwili ya Ligi Kuu England kati ya timu kubwa sita, ina hatihati ya kukosa michuano ya Ulaya msimu ujao kutokana na hali mbaya zilizonazo msimu huu.

Wikiendi hii mechi za Ligi Kuu zinapumzika na kinachoenda kufanyika ni mtifuano wa raundi ya nne ya Kombe la FA na klabu zinawania taji hilo ambalo lina faida kwenye michuano ya kimataifa.

Manchester United na Tottenham ndizo zinazotazamwa zaidi kutokana na mienendo yao kwenye Ligi Kuu na zina nafasi ndogo sana ya kucheza michuano ya Ulaya.

Wababe hawa hawapo hata katika 10 bora, Man United ikiwa nafasi ya 13 na Spurs 14, huku hofu kubwa kwa mashabiki wao ni kutoshiriki kabisa michuano ya kimataifa kwa msimu ujao.

Man United ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 29 ilizokusanya

kwenye mechi 24, ikishinda nane, sare tano na kufungwa 11.

Ili kuonekana katika michuano ya kimataifa kwa msimu ujao, Man United ina njia tatu tu, kwanza ni kuchukua taji la Europa League ambako wapo hatua ya 16 bora hadi sasa na hiyo itawafanya kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na ikishindikana, itatakiwa kuchukua Kombe la FA ambako wapo raundi ya nne na hiyo itawawezesha kufuzu tena kwa staili hiyo Europa League.

Hata hivyo, kucheza michuano ya Europa kwa msimu wa pili mfululizo inaweza kuwa na athari hasi nyingi kwa upande wao hususan dirisha la usajili kwani wachezaji wengi bora wanahitaji kutua timu zinazocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na ili kuwashawishi wajiunge na timu yako badala ya timu hizo zilizopo kwenye mashindano hayo, itahitaji kutoa kiasi kikubwa cha pesa.

Licha ya kufuzu kucheza Europa au Ligi ya Mabingwa Ulaya, Man United inaweza kupambana ili kushiriki walau UEFA Conference League na itawahitaji kumaliza nafasi ya saba katika msimamo wa ligi.

Hadi kufikia sasa timu inayoshikilia nafasi ya saba ambayo ni Bournemouth utofauti wa alama kati yao na wao ni 11.

Hivyo ili kuifikia itahitaji kuendelea kushinda na kuiombea timu hiyo kupoteza mechi nne.

Tottenham ipo nafasi ya 14, nyuma ya Man United na alama 27, baada ya kucheza mechi 24, ikishinda nane, sare tatu na kufungwa 13, namna ya kwanza inayoweza kufanya ili kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kumaliza nafasi nne za juu jambo linawezekana kihesabu ingawa ni ngumu kutokana na alama zake.

Tofauti kati ya Spurs na Chelsea iliyopo nafasi ya nne ni pointi 16 ambazo ili kuifikia itahitaji kuiombea ipoteze mechi tano huku yenyewe ikishinda zote.

Vile vile inaweza kufuzu kwa kushinda Kombe la FA na itakutana na Aston Villa, mchezo unaoonekana kuwa mgumu.

Ikiwa itashindwa kote, inaweza kufuzu kucheza michuano ya Europa kwa kumaliza nafasi ya tano na sita na tofauti ya pointi kati yao na timu zilizopo nafasi hizo (Man City, Newcastle) ni pointi 15 ambazo ili kuzifikia, itatakiwa kuziombea zipoteze mechi nne kati ya tano zijazo.

Michuano ya mwisho ikiwa itashindwa kufuzu kote itakuwa na nafasi ya kwenda Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa itachukua taji la Europa League na imeingia hatua ya 16 bora.