Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United kuna kitu

Muktasari:

  • Kauli hiyo ilitoka baada ya klabu hiyo kumaliza msimu wa Ligi Kuu England vibaya baada ya kuvuna pointi 42 na kushika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi hiyo, huku ikichapwa pia kwenye fainali ya Europa League na Tottenham Hotspur.

MANCHESTER, ENGLAND: “NYAKATI nzuri zinakuja.” Hiyo ilikuwa ahadi ya kocha wa Manchester United, Ruben Amorim baada ya kumalizika kwa msimu uliopita Mei, mwaka huu.

Kauli hiyo ilitoka baada ya klabu hiyo kumaliza msimu wa Ligi Kuu England vibaya baada ya kuvuna pointi 42 na kushika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi hiyo, huku ikichapwa pia kwenye fainali ya Europa League na Tottenham Hotspur.

Usajili wa Pauni 200 milioni kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka huu uliibua matumaini makubwa kwa baadhi ya mashabiki. Lakini, baada ya ushindi mmoja kwenye mechi tatu za ligi - tena ikihitaji bao la penalti kwenye dakika za majeruhi dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu, Burnley, huku ikitoka kutupwa nje ya Kombe la Ligi na timu ya daraja la nne, Grimsby kuliwafanya watu wa huko Theatre of Dreams kuwa na wasiwasi msimu mwingine wenye kumbukumbu mbaya unakwenda kutokea.

Hata hivyo, chini ya kapeti ya mechi hizo tatu za kwanza kwenye ligi, kocha Amorim ni kama vile anapika mambo yake kimyakimya na si muda mrefu, Man United itakuwa tishio kubwa uwanjani.

Kwa sasa watu wamekuwa na mtazamo hasi juu ya mwanzo wa Man United, lakini takwimu za mambo muhimu ya uwanjani zinaonyesha tofauti kabisa, kwamba kuna kitu kinachoonyesha dalili ya kuwa na mwisho mzuri wa kikosi hicho chini ya kocha Amorim.

Man United inashika namba moja kwenye vipengele vyote vinne muhimu kwenye suala la kushambulia. Ipo juu ya Liverpool, juu ya Arsenal, juu ya Chelsea na juu ya Manchester City, ambazo zote kwenye mitazamo ya watu wanaamini ndizo timu zilizoanza msimu vizuri.

Kwanza, Man United imepiga mashuti mengi kuliko timu nyingine yoyote ile kwenye ligi. Takwimu za Opta zinafichua Man United imepiga mashuti 58 - mashuti 14 zaidi ya timu inayofuatia kwa kupiga mashuti mengi kwenye Ligi Kuu England msimu huu ambazo ni Chelsea na Bournemouth.

Pili, Man United imelikaribia zaidi goli la timu pinzani na kugusa mpira mara nyingi ndani ya boksi la wapinzani kuliko timu zote ikifanya hivyo mara 99, huku timu inayofuatia ni Bournemouth iliyogusa mara 87 ndani ya boksi la timu pinzani.

Tatu, Man United pia ina namba nzuri za uwezekano wa kupata bao kwa mechi, ikiwa na alama ya 6.78 ya uwezekano wa kufunga bao kwenye kila mechi kutokana na nafasi inazotengeneza. Lakini, imekuwa na bahati mbaya kwa kutumbukiza mipira hiyo nyavuni -  ikigongesha mwamba wa magoli ya wapinzani mara nne ikiifanya kushika namba moja tu kwa kuwa na bahati mbaya. Kwa timu zote za Big Six, Man United ndiyo imekuwa na bahati mbaya kwenye hilo.

Nne, Man United inashika namba moja pia kwenye ligi kwa timu zilizofanya mashambulizi ya kushtukiza, ikifanya hivyo mara nane, huku ikishika namba mbili kushinda kwa bato za ana kwa ana kwa wachezaji, ikifanya hivyo mara 173 na inashika namba moja kwenye wastani wa asilimia 54.4 wa usahihi wa kupiga krosi kwenye robo tatu ya uwanja kwa pasi zisizokuwa za mipira iliyokufa. Kwa takwimu hizo, kitu kilichobaki kwa Man United ni kufanyia kazi kwenye kutumia nafasi inazozitengeneza na hilo likifanikiwa, chama hilo la Amorim litakuwa balaa uwanjani.

Mtihani mzito upo mbele yao wakati itakapomenyana na Man City, Chelsea na Brentford katika mechi tatu zijazo kwenye Ligi Kuu England baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.