Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United bado inataka kumuuza Rashford

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa vigogo wa Man United wapo tayari kupokea ofa kutoka timu nyingine ikiwa Barca itashindwa kutoa kiasi kinachohitajika ili kumsainisha mkataba wa moja kwa moja staa huyo.

MANCHESTER United haina mpango wa kumrudisha tena Marcus Rashford, 28, kwenye kikosi chao cha kwanza msimu ujao atakapomaliza mkopo wake Barcelona.

Inaelezwa vigogo wa Man United wapo tayari kupokea ofa kutoka timu nyingine ikiwa Barca itashindwa kutoa kiasi kinachohitajika ili kumsainisha mkataba wa moja kwa moja staa huyo.

Kwa mujibu wa watu wa karibu na Rashford, staa huyo mwenyewe anatamani sana kuendelea kusalia Barca akiamini akiwa hapo ataendelea kuonyesha kiwango bora zaidi.

Ikiwa Barca itaendelea kusuasua katika kutoa Pauni 26 milioni ili kumsajili mazima staa huyu kuna uwezekano PSG ikapiga hodi Old Trafford na kutoa takribani mara mbili ya dau hilo ili kumpata mshambuliaji huyo wa England.

Hivi karibuni kulikuwa na minong'ono kutoka kwa mashabiki waliokuwa wanaona huenda staa huyo angerejea tena Man United hususani baada ya kuweka chapisho la kuipongeza timu hiyo baada ya kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu. Mkataba wa sasa wa fundi huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Enzo Fernandez

ARSENAL na Barcelona zinamfuatilia kwa karibu kiungo wa Chelsea, Enzo Fernández, 25,  ili kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hata hivyo, klabu hizo zinakabiliwa na ushindani kutoka Real Madrid ambayo pia inaonekana kuwa chaguo la Enzo mwenyewe. Mbali ya Arsenal, klabu nyingine ya Ligi Kuu England inayotamani kumsajili staa huyu pia ni Manchester City.

Licha ya klabu nyingi kuonyesha nia ya kumsajili staa huyu, taarifa zinadai Chelsea haina mpango wa kumwachia kirahisi, hivyo klabu itakayomhitaji itatakiwa kulipa dau nono ambalo linaweza kuvunja rekodi.


James Trafford

NEWCASTLE United imeweka usajili wa kipa mpya kama moja ya vipaumbele vyao vikubwa dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuona nafasi hiyo ina udhaifu.

Miongoni mwa makipa wanaowatazama ni pamoja James Trafford, 23, kutoka kwa Manchester City na Bart Verbruggen, 23, wa Brighton.

Trafford anachukuliwa kama kipa mwenye uwezo mkubwa na kuipata saini yake inaonekana kuna ugumu kwa asilimia kadhaa kutokana na umuhimu wake katika kikosi cha Man City ingawa anatumika kama kipa namba mbili nyuma ya Gianluig Donnarumma.


Jannik Schuster

BRENTFORD ipo katika harakati za kukamilisha usajili wa beki wa Red Bull Salzburg na Austria, Jannik Schuster, 19, kuelekea dirisha lijalo.

Inaripotiwa dili hilo linaweza kufikia thamani ya Pauni 17 milioni kiasi ambacho Salzburg imesisitiza kwamba hakipungui.

Schuster ni mmoja wa wachezaji vijana wanaochipukia na amezivutia klabu kadhaa kutokana na uwezo wake na utulivu akiwa na mpira mguuni.


Jan Paul van Hecke

TOTTENHAM Hotspur imevutiwa na beki wa kati wa Brighton, Jan Paul van Hecke, 25, na inahitaji kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hata hivyo, Spurs inakabiliwa na ushindani mkali kutoka Chelsea Fna Liverpool , ambazo pia zinamfuatilia beki huyo.

Ripoti zinadai Brighton haina mpango wa kumuuza staa huyu kwa sasa ingawa inaweza kufanya hivyo ikiwa itapokea ofa nono. Mkataba wake unamalizika mwaka 2027.


Wesley Fofana

WAKALA wa Wesley Fofana, 25, yupo katika mazungumzo na Barcelona inayohitaji kumsajili staa huyo wa Chelsea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa, hivi karibuni amekuwa na panda shuka nyingi kutokana na majeraha ya mara kwa mara.

Hata hivyo, dili hilo linategemea na kiasi ambacho Chelsea itakihitaji ili kumuuza kwani Barca imeweka wazi kwa wakala wake hawatotoa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kumnunua. Tangu kuanza kwa msimu huu, Fofana amecheza mechi 34 za michuano yote.


El Hadji Malick Diouf

MANCHESTER United inamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto wa West Ham na timu ya taifa ya Senegal, El Hadji Malick Diouf, 21, ambaye inahitaji kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Lengo la Man United ni kuongeza ushindani katika nafasi ya beki wa kushoto na Luke Shaw, 30, amekuwa chaguo namba moja. Diouf anaonekana kulivutia zaidi benchi la ufundi la Man United ambalo linaamini atatumika kwa muda mrefu.


Hidemasa Morita

LEEDS United imefikia hatua nzuri katika mchakato wao wa kutaka kumsajili kiungo mkabaji wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Japan, Hidemasa Morita, 30.

Inaelezwa Morita yuko tayari kujiunga na Leeds iwapo klabu hiyo itahakikisha inabaki Ligi Kuu England msimu ujao.

Licha ya umri kuwa unaenda kumtupa mkono Morita ana uzoefu wa kutosha ambao ndio umewapagawisha mabosi wa Leeds ambao wanaamini utaongeza kitu katika kikosi chao.