Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matano Thunder vs Timberwolves

Muktasari:

  • Hicho kilikuwa kiwango cha timu iliyokuwa na kiu ya ushindi. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Oklahoma City Thunder, timu ya msimu yenye ushindi mara 68 iliyoongoza Kanda ya Magharibi na tayari ikiwa mbele kwa 3-1 katika fainali ya hiyo.

OKLAHOMA, MAREKANI: KULIKUWA na mitego mikali ya kudaka mpira, kupora na baadaye danki za maana yaani aina ya kutupia mipira kwenye kikapu kwa nguvu na ustadi kwa kuruka na kuushindilia mpira moja kwa moja nyavuni.

Hicho kilikuwa kiwango cha timu iliyokuwa na kiu ya ushindi. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Oklahoma City Thunder, timu ya msimu yenye ushindi mara 68 iliyoongoza Kanda ya Magharibi na tayari ikiwa mbele kwa 3-1 katika fainali ya hiyo.

Thunder ilikuwa na hamu ya kufuzu mapema na kutimiza lengo lake msimu huu. Na ilifanya hivyo kwa kishindo. Haikuwa mechi ya kusisimua. Thunder ilionyesha ubora bila chembe ya shaka ikiifunga Minnesota Timberwolves kwa alama 124-94 katika mchezo wa fainali wa tano. Ushindi huo uliiahakikishia nafasi ya kucheza tena fainali za NBA kwa mara ya pili katika historia - mara ya kwanza tangu 2012.

Kwa jinsi Thunder ilivyoanza msimu Oktoba hakuna anayeshangazwa na mafanikio hayo. Hadi sasa ndio timu bora zaidi iliyosalia. Na kama hali itaendelea ilivyo huenda ikawa bingwa mwisho msimu huu.

Supastaa Shai Gilgeous-Alexander aling'ara tena akibeba tuzo ya Mchezaji Bora wa Fainali za Magharibi akisaidiwa ipasavyo na Jalen Williams, Chet Holmgren, Alex Caruso na wengineo.

Kocha wa timu hiyo Mark Daigneault anasema: “Tulikuwa bora kila sehemu, tulilinda vizuri, tulisaidiana na tulijibu kila mpango waliokuwa nao (wapinzani wao). Huu ulikuwa mchezo wa kufuzu fainali na wachezaji walikuwa na umakini wa hali ya juu.” Haya ndiyo mambo matano muhimu yaliyojitokeza katika ushindi wa Thunder dhidi ya Wolves


1. Big 3 mpya

Mara ya mwisho Thunder ilipofika fainali ilikuwa 2012, ikiwa na kikosi cha nyota wachanga kama Kevin Durant, Russell Westbrook na James Harden. Lakini, sasa miaka 13 baadaye majina mapya yamechukua nafasi hiyo yakiwa ni Shai, Chet na J-Dub (Jalen Williams). Nyota hao wameonyesha uwezo mkubwa wakicheza kwa kuaminiana, huku wakisaidiana kushambulia kutoka pande zote za uwanja. Shai tayari ni mshindi wa tuzo ya MVP wa msimu wakati Holmgren analinda vizuri na kutengeneza nafasi kwa mitupo ya mbali ilhali Williams amekuwa msaada mkubwa katika kila hatua ya mchezo.


2. Msimu wa Shai

Huyu mtu ni kiongozi wa timu yenye ushindi 68?, nyota wa All-Star?, Mfungaji bora wa msimu?, First-Team All-NBA?, MVP wa NBA? na MVP wa Fainali za Magharibi? Sasa basi elewa kwamba Shai amekuwa na msimu wa kutisha. Katika mchezo wa kufuzu alitupia pointi 34. Huo ni mfano wa pili kwake kung’ara katika mechi ya kufunga mfululizo kwani awali alivuna pointi 35 dhidi ya Nuggets kwenye mchezo wa saba wa nusu fainali.


3. Anthony Edwards

Kufika fainali za kanda mara mbili mfululizo akiwa na umri wa miaka 23 ni mafanikio ya pekee kwa Anthony Edwards. Hata hivyo, alikutana na kipimo bora kutoka kwa nyota waliokomaa kama Shai na Luka Doncic. Hilo linapaswa kuwa funzo. Edwards ana kipaji cha hali ya juu akiwa na uwezo wa kufunga kwa mikono yote miwili na ni mchezaji mzuri wa mitupo ya mbali. Lakini, bado hajaifikia hadhi ya kuwa kati ya wachezaji bora zaidi. Katika safu hii alikosekana wakati mwingine muhimu, na japo ulinzi wa Thunder ulikuwa madhubuti, Edwards pia alionekana kushindwa kujibu mapigo.


4. Randle na Reid

Majira ya joto yanakuja na maswali mazito kwa Minnesota Timberwolves ni juu ya mabadiliko ya umiliki iwapo yatakamilika na kama Marc Lore na Alex Rodriguez watachukua rasmi. Uamuzi wa mwanzo utategemea hali ya wachezaji huru kama Julius Randle (anaweza kuchagua kuondoka), Naz Reid na Nickeil Alexander-Walker. Kuendelea nao wote kutagharimu fedha nyingi na kuiweka klabu kwenye wakati mgumu wa ulipaji kodi inayojulikana kama “second apron”. Randle ndiye kiini. Alitoka New York Knicks kupitia dili la Karl-Anthony Towns. Kama Wolves haitamsainisha dili jipya itakuwa imepoteza mali bila faida.

Kama itaendelea na Naz Reid itaingia gharama kubwa ya kuwa na nyota wawili wanaocheza eneo la kati pamoja na Rudy Gobert. Kwa upande mwingine mkataba wa Nickeil unaweza kuvuka mipaka ya kodi ya kifedha.


5. Ulinzi Thunder

Ni lazima ielezwe kwamba silaha kubwa ya Thunder ni uwezo wa kukabiliana na silaha za wapinzani wao. Katika robo ya kwanza ya mchezo wa tano, Wolves ilifunga mara tatu huku ikipoteza mipira minne. Thunder ilimaliza mchezo mapema kwa kuwa na ulinzi bora. Kocha Daigneault anasema: “Hii ilikuwa nusu ya kwanza yenye ulinzi bora zaidi tuliyowahi kucheza.”  Wolves walipata pointi tisa katika robo ya kwanza kwenye mechi ya kuamua hatma.