Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luka Modric afungua milango kutua AC Milan

TETESI Pict

Muktasari:

  • Modric, 39, ataachana na Real Madrid baada ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani, ambapo atakuwa amehitimisha miaka 13 ya kuitumikia miamba hiyo ya Hispania.

AC Milan imepokea taarifa muhimu kutoka kwa kiungo veterani Luka Modric kwamba milango wazi kwenda kujiunga na miamba hiyo ya Italia.

Modric, 39, ataachana na Real Madrid baada ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani, ambapo atakuwa amehitimisha miaka 13 ya kuitumikia miamba hiyo ya Hispania.

Modric anakaribia kufikisha umri wa miaka 40, lakini, hajapanga kutundika daruga, akilenga kuendelea kukipiga ili aitumikie Croatia kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.

Staa huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur alionyesha kiwango bora msimu uliopita, alipotumika kwenye mechi 56 Real Madrid chini ya kocha Carlo Ancelotti, ambapo alifunga mabao manne na kuasisti mara tisa. Modric anatarajiwa kubaki Ulaya.


Kepa Arrizabalaga

ARSENAL ipo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kipa wa Chelsea, Mhispania Kepa Arrizabalaga, 30, katika dirisha hili ambapo itahitajika kutoa Pauni 5 milioni kama ada ya uhamisho. Kepa anasajiliwa kwa ajili ya kwenda kumpa ushindani zaidi David Raya ambaye ndiye kipa namba moja kwa sasa. Akiwa kwa mkopo Bournemouth msimu uliopita, kipa huyu alionyesha kiwango bora.


Anthony Elanga

NEWCASTLE United imeripotiwa kumfukuzia winga wa Nottingham Forest, Anthony Elanga ikihitaji huduma yake kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya. Newcastle imevutiwa na ubora wa staa huyo wa zamani wa Manchester United na ndiyo maana inahitaji saini yake ili akakipige St James’ Park msimu ujao, ambapo miamba hiyo itakuwa bize kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Maxime Esteve

BURNLEY inataka Pauni 50 milioni ili kumuuza beki wa kati raia wa Ufaransa, Maxime Esteve, 23, ambaye anahitajika na timu kibao hususani Bayern Munich. Inaelezwa Bayern imetua mezani kwa ajili ya kumsajili staa huyo baada ya ripoti ya kocha Vincent Kompany kumtaja. Kompany aliwahi kumfundisha staa huyo wakati akiinoa Burnley.


Nico Williams

BAYERN Munich inatafuta winga na miongoni mwa mastaa ambao tayari imeshawaweka katika rada ni winga wa PSG na Ufaransa, Bradley Barcola, 22, na wa Athletic Bilbao, Nico Williams. Bayern inataka kuboresha kikosi zaidi kwa ajili ya kuhakikisha msimu ujao inafanya vizuri kwenye michuano ya ndani na kimataifa baada ya kutofanya vizuri msimu uliopita.


Illia Zabarni

MABOSI wa Bournemouth wameiambia PSG kuwa itahitajika kutoa kiasi kisichopungua Pauni 59 milioni ili kuipata saini ya beki wa kati raia wa Ukraine, Illia Zabarni, katika dirisha hili la majira ya kiangazi. Zabarni mwenye umri wa miaka 22, amezivutia timu nyingi huko Ulaya kutokana na mchango mkubwa alioutoa akiwa na Bournemouth msimu uliomalizika, ambapo alikuwa miongoni mwa mastaa kikosini.


Antoine Semenyo

TOTTENHAM Hotspur imeingia katika vita dhidi ya Manchester United ili kuipata saini ya mshambuliaji wa  Bournemouth, Antoine Semenyo, katika dirisha hili la majira ya kiangazi huko Ulaya. Supastaa huyo wa kimataifa wa Ghana mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akiwindwa na vigogo wengi tangu dirisha la majira ya baridi mwaka huu.


Mohammed Kudus

NEWCASTLE United imefikia hatua nzuri katika mazungumzo na wawakilishi wa winga wa West Ham United, Mohammed Kudus, 24, ambaye inataka kumsajili katika dirisha hili baada ya kushindwa kuipata saini ya straika wa Brentford, Bryan Mbeumo anayeonekana kuwa karibu zaidi kujiunga na Manchester United.