Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lopez afunga hat trick, Rashford mbili Barca ikipiga mtu sita

Muktasari:

  • Lopez aliiweka Barcelona mbele kwa mabao mawili kipindi cha kwanza akimalizia kwa ustadi, kabla ya kuongeza la tatu, penalti ya Lamine Yamal na mabao mawili ya Rashford kukamilisha ushindi mkubwa licha ya juhudi za muda mfupi za Olympiacos kurejea mchezoni.

BARCELONA, HISPANIA: Fermin Lopez amefunga mabao matatu huku Marcus Rashford akiendeleza makali yake kwa kufunga mara mbili, akiifikisha jumla ya mabao manne katika mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati Barcelona ikiizidi nguvu Olympiacos kwa ushindi wa mabao 6-1, mechi ikichezwa Estadi Olímpic Lluís Companys, Hispania, usiku wa Oktoba 21, 2025.

Lopez aliiweka Barcelona mbele kwa mabao mawili kipindi cha kwanza akimalizia kwa ustadi, kabla ya kuongeza la tatu, penalti ya Lamine Yamal na mabao mawili ya Rashford kukamilisha ushindi mkubwa licha ya juhudi za muda mfupi za Olympiacos kurejea mchezoni.

Baada ya dakika saba tu, Lopez alimuwekea Yamal pasi nzuri iliyomuweka pekee langoni, na aliporejea eneo la hatari, alifunga kwa urahisi baada ya kipa Konstantinos Tzolakis kushindwa kudhibiti mpira uliorudi.

Kiungo huyo wa Hispania aliongeza bao la pili dakika ya 30 baada ya kukimbia kwenye nafasi nzuri kufuatia pasi ya Dro Fernandez, akapiga mguu wa kushoto uliokunja na kuingia kona ya kushoto ya goli.

Kipindi cha pili kilianza kwa hali ya ajabu. Ayoub El Kaabi alidhani amepunguza pengo kwa kichwa, lakini baada ya marejeo kupitia VAR, refa Urs Schnyder alifuta bao hilo kwa kosa la kuotea na badala yake akaipa Olympiacos penalti kwa sababu ya handball iliyofanywa na Eric Garcia ambayo El Kaabi aliitumia vyema kwa mpira uliogonga mwamba na kuingia wavuni.

Dakika tatu baadaye, kiungo wa Olympiacos, Santiago Hezze alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kumgonga Lopez kwa mkono usio na udhibiti.

Usiku huo pia ulikuwa wa kihistoria kwa Lamine Yamal, ambaye alifikisha mechi 25 za Ligi ya Mabingwa akiwa na umri wa miaka 18 na siku 100, rekodi ya umri mdogo zaidi. Yamal alifunga penalti kwa utulivu baada ya Rashford kuchezewa vibaya alipokuwa akijaribu kumzunguka kipa Tzolakis.

Barcelona haikuridhika, iliendelea kushambulia kwa zaidi kusaka mabao. Dakika ya 74, Rashford alifunga bao lake la kwanza kwa shuti la chini, na dakika mbili baadaye Lopez akapiga kwa nguvu mpira pembezoni mwa eneo la hatari, akawa Mhispania wa kwanza kufunga hat-trick kwenye Ligi ya Mabingwa akiwa na Barcelona.

Rashford aliongeza bao lake la pili kwa shuti kali baada ya kudhibiti mpira mrefu kwa ustadi mkubwa. Wakati akiwa Manchester United, alifunga zaidi ya bao moja katika mechi moja ya Ligi ya Mabingwa mara moja pekee, lakini tayari ameweza kufanya hivyo mara mbili akiwa na Barcelona.

Hii ilikuwa mara ya kwanza tangu ushindi wao maarufu wa 6-1 dhidi ya Paris Saint-Germain mwaka 2017 ambapo Barcelona imefunga mabao sita katika mechi ya Ligi ya Mabingwa.

Barcelona sasa ina alama sita baada ya mechi tatu, ikishinda dhidi ya Newcastle (2-1) na kupoteza kwa PSG kwa matokeo sawa.

Olympiacos inabaki na alama moja pekee, na sasa imepoteza mechi 12 mfululizo za ugenini kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.