Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yawasilisha ofa mpya kwa Florian Wirtz

TETESI Pict

Muktasari:

  • Wirtz ambaye ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Leverkusen, anadaiwa kuwaambia vigogo wa klabu hiyo kwamba anataka kuondoka.

LIVERPOOL iko tayari kutoa ofa ya mwisho yenye thamani ya Pauni 118 milioni kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani, Florian Wirtz, mwenye umri wa miaka 22, baada ya ofa yao ya kwanza ya Pauni 113 milioni kukataliwa.

Wirtz ambaye ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Leverkusen, anadaiwa kuwaambia vigogo wa klabu hiyo kwamba anataka kuondoka.

Katika msimu uliopita Wirtz alicheza mechi 45 za michuano yote na akahusika katika mabao 31, akifunga mabao 16 na kutoa asisti 15.

Leverkusen inadaiwa kuhitaji zaidi ya Pauni 125 milioni kama ada yake uhamisho, kiasi ambacho Liverpool inaona ni kikubwa na badala yake imefikia kutaka kutoa hiyo Pauni 118 milioni.

Mkataba wa sasa wa Wirtz unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Jack Grealish

EVERTON ina mpango wa kumsajili kiungo wa Manchester City na England, Jack Grealish, katika dirisha hili la majira ya kiangazi lakini kwa uhamisho wa mkopo.

Grealish ambaye ameonyeshwa mkono wa kwaheri na Man City, msimu uliopita alicheza mechi 32 za michuano yote na  kufunga mabao matatu. Muda mwingi aliishia benchini.


Martin Zubimendi

REAL Madrid inapanga kufanya jaribio la mwisho kumsajili kiungo wa Real Sociedad na Hispania, Martin Zubimendi, mwenye umri wa miaka 26, ambaye yuko karibu kujiunga na Arsenal.

Madrid imejiingiza katika dili hilo hivi karibuni lakini tayari Zubimendi anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kujiunga na Arsenal ambayo alianza kufanya nayo mazungumzo tangu mwaka jana.


Benjamin Sesko

ARSENAL bado inaendelea kufanya mazungumzo na RB Leipzig ili kuipata saini ya straika wa kimataifa wa Slovenia, Benjamin Sesko, mwenye umri wa miaka 22, ambaye  shida kubwa inayokwamisha dili lake ni ada ya uhamisho.

Inaelezwa kiasi cha pesa ambacho Leipzig inakihitaji, Euro 80 milioni, ni kikubwa zaidi ya kiwango kile ambacho Arsenal iko tayari kukitoa.


Rasmus Hojlund

MSHAMBULIAJI wa Manchester na timu ya taifa ya Denmark, Rasmus Hojlund, 22, amesema hafikirii kuondoka Manchester United, licha ya kuhusishwa na uhamisho wa kujiunga na Inter Milan.

Hojlund ambaye ni mmoja kati ya mastaa waliopata muda mwingi wa kucheza katika kikosi cha Man United, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Mike Maignan

CHELSEA iko tayari kulipa euro 15 milioni kwenda AC Milan kwa ajili ya kumsajili kipa wa timu hiyo na Ufaransa mwenye umri wa miaka 29, Mike Maignan katika dirisha hili.

Maignan ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani, msimu uliopita alicheza mechi 53 za michuano yote.


Victor Osimhen

MSHAMBULIAJI wa Napoli na Nigeria, Victor Osimhen amekataa mkataba wa Euro 30 milioni aliowekewa mezani na  Al-Hilal katika dirisha hili.

Al-Hilal ilikuwa imeshafanya makubaliano na Napoli na ilikuwa tayari kulipa Euro 75 milioni ili kumpata staa huyu ambaye hapo awali ripoti zilieleza kwamba amekubali kujiunga nayo.


Jadon Sancho

WINGA wa Manchester United na England, Jadon Sancho, 25, anatakiwa na Al-Hilal.

Sancho ambaye msimu uliopita alikuwa akicheza kwa mkopo Chelsea, mkataba wake na Man United unatarajiwa kumalizika mwakani.

Msimu uliopita akiwa kwa mkopo alicheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao matano.