Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool sasa yapanga kumng’oa Nkunku Chelsea

Muktasari:

  • Nkunku ambaye ni mshambuliaji namba mbili kwenye kikosi cha Chelsea ameomba kuondoka mara baada ya msimu huu kumalizika ili kujiunga na timu itakayomhakikishia namba katika kikosi cha kwanza.

RIPOTI zinaeleza mshambuliaji wa Chelsea, Christopher Nkunku, mwenye umri wa miaka 27, ni moja kati ya mastaa ambao Liverpool inataka kuwasajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa itaachana na Darwin Nunez anayehusishwa na timu mbalimbali za ndani na nje ya bara la Ulaya.

Nkunku ambaye ni mshambuliaji namba mbili kwenye kikosi cha Chelsea ameomba kuondoka mara baada ya msimu huu kumalizika ili kujiunga na timu itakayomhakikishia namba katika kikosi cha kwanza.

Nkunku ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, taarifa zinaeleza anaweza kuuzwa kwa kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni.

Mabosi wa Liverpooil wamevutiwa sana na fundi huyu kutokana na uwezo wake wa kufunga aliouonyesha akiwa na Chelsea licha ya kutopata nafasi ya kutosha. Msimu huu amefunga mabao 14 katika mechi 42 za michuano yote.


Adam Wharton

LIVERPOOL imeingia katika vita dhidi ya  Real Madrid na Barcelona kwa ajili ya kuwania kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace na England, Adam Wharton, mwenye umri wa miaka 21, anayekadiriwa kugharimu Pauni 60 milioni.

Adam ameonyesha kiwango sana msimu huu kiasi cha kuzivutia timu nyingi.  Palace inadaiwa kuwa tayari kumuuza kwa timu itakayotoa kiasi sahihi cha pesa.


Harvey Elliott

WOLVES inapambana sana kuhakikisha inaipata huduma ya kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Harvey Elliott, mwenye umri wa miaka 22.

Elliot anataka kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Liverpool.

Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

Rodrygo

VIGOGO watatu kutoka Ligi Kuu England ambao ni Chelsea, Manchester City, na Arsenal tayari wameanza mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, ambaye amepoteza nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Bernabeu.

Rodrygo anadaiwa kutaka kuondoka kwa sababu haoni kama anapewa heshima ndani ya timu hiyo.


Axel Disasi

ASTON Villa inataka kumsainisha mkataba wa kudumu beki wa Chelsea, Axel Disasi, 27, ambaye anacheza kwa mkopo katika kikosi chao msimu huu.

Mabosi wa Villa wamevutiwa sana na kiwango alichoonyesha Disasi tangu ajiunge nao. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu huu amecheza mechi 27 za michuano yote.


Marc Guehi

CHELSEA imewaweka katika orodha yake mabeki wawili ambao ni Jarrad Branthwaite, 22, kutoka Everton na Marc Guehi, wa Crystal Palace ikihitaji kuwasajili katika dirisha lijalo.

Kocha Enzo Maresca anahitaji huduma ya beki mmoja kati ya hawa au wote ili kuboresha eneo la ulinzi. Wachezaji hawa wote wameonyesha kuwa hawana mpango wa kuendelea kusalia kwenye timu zao.


Ferran Torres

ASTON Villa inataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Ferran Torres, mwenye umri wa miaka 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Taarifa zinaeleza, Villa ipo tayari kutoa kiasi kisichopungua Pauni 42 milioni. Mkataba wa sasa wa Ferran unatarajiwa kumalizika mwaka 2027


James Milner

BRIGHTON imefikia hatua nzuri kwenye mazungumzo na kiungo wake mkongwe raia wa England, James Milner, 39, inayehitaji kumpa mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia. Vigogo wa Brighton wanatamani staa huyu aongeze mkataba mpya kutokana na mchango wake licha ya kutokuwa chaguo la kwanza la kocha. Mkataba unaisha Juni.