Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool kumrudisha Klopp kwa muda! Enrique awekwa kwenye orodha

LIVERPOOL Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa The Sun, Liverpool imewasilisha ombi hilo kwa Klopp mwenye umri wa miaka 58, ikiamini kocha huyo kutoka Ujerumani ataweza kuinusuru timu yao katika kipindi hiki, ambacho imekua haifanyi vizuri katika mechi za Ligi Kuu ya EPL na zile za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Klabu Liverpool imemuomba kocha Jürgen Klopp, kurejea klabuni hapo kwa muda ili kuchukua nafasi ya Arne Slot, aliyekalia kuti kavu kwa sasa.

Kwa mujibu wa The Sun, Liverpool imewasilisha ombi hilo kwa Klopp mwenye umri wa miaka 58, ikiamini kocha huyo kutoka Ujerumani ataweza kuinusuru timu yao katika kipindi hiki, ambacho imekua haifanyi vizuri katika mechi za Ligi Kuu ya EPL na zile za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LIVER 01

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, endapo Klopp ambaye kwa sasa ni mkuu wa kimataifa wa soka wa kampuni ya Red Bull atakubali ombi hilo, atapewa mkataba hadi mwishoni mwa msimu huu, huku uongozi wa Liverpool ukiandaa mkakati wa muda mrefu wa kumpa ajira Luis Enrique, ambaye ni kocha wa mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain.

Slot yuko kwenye hatari ya kupoteza kazi huko Anfield, baada ya kikosi chake kupoteza mechi tisa kati ya 12 katika mashindano yote, hali ambayo imezua wasiwasi kwenye uongozi wa Liverpool. 

LIVER 03

Hata hivyo Slot anasisitiza kuwa bado anaungwa mkono na wamiliki wa wa klabu hiyo Fenway Sports Group, licha ya mazingira mabaya yanayomzunguuka.

Kocha huyo raia wa Uholanzi, amesema mazungumzo kati yake na viongozi wa klabu yamekuwa yakiendelea muda wote katika kipindi hiki kigumu, ambacho kilizidi kuwa kibaya zaidi juzi Jumatano, Novemba 26, 2025 baada ya kupoteza mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven kwa mabao 4–1 kwenye dimba la Anfield.

LIVER 02

 “Mazungumzo ni yale yale tuliyokuwa tukifanya tangu nimefika hapa, sawa na yale ya kipindi cha mwaka na nusu uliopita,” amesema Slot.

Hata hivyo, The Sun imeeleza kuwa mazungumzo mengine yamekuwa yakiendelea miongoni mwa viongozi wa Liverpool, ambao wana wasiwasi kuwa Slot anapoteza ushawishi kwa wachezaji siku hadi siku.