Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa umeme... Everton 1, Arsenal 2

UMEME Pict
UMEME Pict

Muktasari:

  • Katika baadhi ya matukio, timu zote mbili zinapopoteza wachezaji kwa kadi nyekundu na kubaki na wachezaji 10 kila upande, mchezo unaweza kuwa wa aina yake, wenye vurugu za kiufundi na burudani kubwa.

LONDON, ENGLAND: LICHA ya kadi nyekundu wakati mwingine kuvuruga mtiririko wa mchezo na kuifanya timu iliyopungukiwa mchezaji kujikita zaidi katika kujilinda, adhabu hiyo pia huongeza msisimko na ushindani ndani ya uwanja.

Katika baadhi ya matukio, timu zote mbili zinapopoteza wachezaji kwa kadi nyekundu na kubaki na wachezaji 10 kila upande, mchezo unaweza kuwa wa aina yake, wenye vurugu za kiufundi na burudani kubwa.

Katika michezo ya Ligi Kuu England iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, wachezaji watatu walionyeshwa kadi nyekundu. Wachezaji hao ni Leny Yoro wa Manchester United, Costinha wa Brighton na James Tarkowski wa Everton.

Hata hivyo, takwimu za Transfermarkt zimeonyesha ni timu zipi zimekuwa zikiongoza kwa kupokea kadi nyingi nyekundu tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu England msimu wa 1992/93.

UME 01

EVERTON YAONGOZA, ARSENAL YA PILI

Everton inaongoza katika orodha hiyo baada ya kufikisha jumla ya kadi nyekundu 114 katika misimu 35 iliyoshiriki Ligi Kuu England. Kadi nyekundu aliyoonyeshwa beki wake James Tarkowski imeifanya timu hiyo kufikisha idadi hiyo na kuiacha Arsenal kwa kadi nne.

Arsenal inashika nafasi ya pili ikiwa na kadi nyekundu 109 tangu msimu wa 1992/93, huku

Chelsea ndiyo timu nyingine pekee iliyovuka alama ya kadi nyekundu 100, ikiwa imepokea 101.

Katika orodha hiyo Newcastle United inashika nafasi ya nne ikiwa na kadi nyekundu 98 katika misimu 32, ikiwa ndiyo timu ya kwanza katika orodha hiyo ambayo haijashiriki kila msimu wa Ligi Kuu England ilhali West Ham United inakamilisha tano bora ikiwa na kadi nyekundu 87 katika misimu 30 iliyoshiriki ligi hiyo.

Nje ya tano bora kuna Tottenham Hotspur inayoshika nafasi ya sita ikiwa na kadi 84, ikifuatiwa na Manchester United katika nafasi ya saba yenye 79.

Manchester City inashika nafasi ya nane ikiwa na kadi nyekundu 78 katika misimu 30, ikifuatiwa na Blackburn Rovers inayoshika nafasi ya tisa ikiwa na kadi 77 katika misimu 18 pekee, ikiwa na rekodi isiyoridhisha ya nidhamu ikilinganishwa na idadi ya misimu iliyoshiriki ligi hiyo.

Aston Villa inakamilisha 10 bora ikiwa na kadi nyekundu 72 katika misimu 32.


UME 02

LIVERPOOL YA 11, CRYSTAL PALACE 19

Liverpool ndiyo timu iliyoshiriki kila msimu wa Ligi Kuu England yenye idadi ndogo zaidi ya kadi nyekundu katika orodha hiyo, ambapo imepokea kadi nyekundu 70 katika misimu yake yote 35 ya kushiriki ligi hiyo, ikiishia nafasi ya 11.

Sunderland inashika nafasi ya 12 ikiwa na kadi 67 katika misimu 18, huku Southampton ikiwa ya 13 kwa kadi 66 katika misimu 25. Leicester City inashika nafasi ya 14 ikiwa na kadi 52 katika misimu 18, huku Fulham ikikamilisha 15 bora ikiwa na kadi 50 katika misimu 20.

Timu nyingine zinazokamilisha orodha ya 20 bora ni Bolton Wanderers na Middlesbrough ambazo kila moja imepokea kadi nyekundu 44, huku Bolton ikiwa katika nafasi ya 16 baada ya kushiriki misimu 13, na Middlesbrough ikiwa ya 17 baada ya misimu 15.

Nayo Leeds United inashika nafasi ya 18 ikiwa na kadi 38 katika misimu 17, Crystal Palace ni ya 19 ikiwa nazo 37 katika misimu 18, huku Wolverhampton Wanderers ikifunga orodha ya 20 bora ikiwa na kadi 33 katika misimu 12.


TIMU 20 ZENYE KADI NYEKUNDU NYINGI EPL

Everton                       114

Arsenal                       109

Chelsea                       101

Newcastle       98

West Ham        87

Tottenham       84

Man United      79

Man City                      78

Blackburn       77

Aston Villa       72

Liverpool                     70

Sunderland     67

Southampton  66

Leicester City 52

Fulham            50

Bolton              44

Middlesbrough            44

Leeds United   38

Crystal Palace            37

Wolverhampton          33