Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kompyuta imetaja hawa hapa usajili Big Six

Muktasari:

  • Sasa mashabiki kwa sasa wanajadili kuhusu timu zao ni wachezaji gani itawanasa na wale itakaowafungulia mlango wa kutokea kwenye dirisha hili ili kuunda vikosi vitakavyochuana kwenye mbio zote.

LONDON, ENGLAND: USAJILI wa dirisha la Januari limejaa mambo mengi kwenye Ligi Kuu England wakati timu mbalimbali zikipambana kuboresha vikosi vyao ili kuja na nguvu mpya katika mchakamchaka wa kusaka matokeo mazuri hadi mwisho wa msimu.

Sasa mashabiki kwa sasa wanajadili kuhusu timu zao ni wachezaji gani itawanasa na wale itakaowafungulia mlango wa kutokea kwenye dirisha hili ili kuunda vikosi vitakavyochuana kwenye mbio zote.

Hata hivyo, hakuna anayefahamu usajili sahihi unaopaswa kufanywa na timu zao na kutokana na hilo, teknolojia imeamua kutumika kutambua ni wachezaji gani sahihi wanaopaswa kunaswa na timu za Big Six kwenye Ligi Kuu England. Hili hapa chaguo la Akili Mnemba (IA) juu ya wachezaji watatu wanaopaswa kusajiliwa na kila timu za Big Six kwenye dirisha hili la majira ya baridi ili kuunda vikosi vya kibabe...


-Arsenal

Jeremie Frimpong

(Bayer Leverkusen)

Rayan Cherki (Lyon)

Evan Ndicka (Roma)

Arsenal imekuwa ikiripotiwa kuhitaji straika mpya msimu huu, lakini AI haiamini kama ishu ya kutafuta mfungaji ni kipaumbele kikubwa kwa timu hiyo. Kwenye orodha ya wachezaji watatu waliochaguliwa na AI ambao Arsenal inapaswa kuwasajili kama inataka kuwa bora, Cherki wa Lyon ndiye pekee mshambuliaji.


-Chelsea

Marc Guehi

(Crystal Palace)

Lautaro Martinez

(Inter Milan)

Victor Osimhen (Napoli)

Usajili wa Marc Guehi una mantiki kwa Chelsea, lakini bila shaka timu yake ya Crystal Palace itahitaji dau kubwa sana. Shida ya mabeki imewafanya Chelsea kumrudisha Trevoh Chalobah aliyekuwa kwa mkopo, huku AI imewachagulia nyota wengine wa kunaswa na The Blues ni mastraika Osimhen na Martinez.


-Liverpool

Alphonso Davies

(Bayern Munich)

Stefanos Tzimas

(FC Nurnberg)

Joao Gomes (Wolves)

Ripoti zinafichua Alphonso Davies anakaribia kusaini mkataba mpya Bayern Munich, lakini AI imemtaja beki huyo wa Canada kama chaguo bora la kufanywa na Liverpool kwenye usajili wao, huku ikiwataja wachezaji wengine wanaopaswa kutua Anfield kuwa ni straika Stefanos Tzimas na Joao Gomes.


-Man City

Florian Wirtz

(Bayer Leverkusen)

Ederson (Atalanta)

Joao Palhinha

(Bayern Munich)

AI imetoa orodha ya wachezaji matata kabisa ambao inaamini watakwenda kuboresha kiwango cha Manchester City, lakini kuwanasa mastaa hao dirisha hili la Januari ni kazi ngumu. Man City imeshawasajili Abdukodir Kusanov na Vitor Reis na inakaribia kumchukua Omar Marmoush dirisha hili.


-Man United

Viktor Gyokeres (Sporting CP)

Randal Kolo Muani (PSG)

Milos Kerkez

(Bournemouth)

Ruben Amorim anahitaji kusajili na anahitaji straika. Lakini, hatampata Randal Kolo Muani kwa sababu ameshakwenda kwa mkopo Juventus licha ya AI kumpendekeza mchezaji huyo kwa miamba ya Old Trafford. Straika Gyokeres tayari yupo kwenye mipango huko Man United na inaweza kumchukua pia Kerkez.


-Tottenham

Illya Zabarnyi

(Bournemouth)

Valentin Arangana (Reimes)

Davide Frattesi

(Inter Milan)

Tottenham Hotspur imekuwa kwenye kipindi kigumu kutokana na wachezaji wake wengi kuwa majeruhi.

Katika kuweka mambo sawa katika kikosi hicho, AI imependekeza Spurs kunasa mastaa watatu ambao wakinaswa na Ange Postecoglou watakuja kubadili mambo kwenye kikosi hicho cha London.