Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa Yanga aitabiria taji Morocco AFCON 2025

Muktasari:

  • Fainali hizo za 35 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1957 zinashirikisha timu za nchi 24 na zitafikia tamati Januari 18 katika taifa hilo la Afrika Kaskazini.

KOCHA mkuu wa zamani wa Yanga, Luc Eymael, amewatabiria wenyeji Morocco nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 michuano inayoanza rasmi kesho Jumapili nchini humo.

Fainali hizo za 35 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1957 zinashirikisha timu za nchi 24 na zitafikia tamati Januari 18 katika taifa hilo la Afrika Kaskazini.

Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano haya kuchezwa kipindi cha Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.

Mashindano hayo yatawakutanisha timu bora kutoka Afrika, akiwemo Tunisia, inayoshiriki kwa mara ya 22 na kuendelea kuweka rekodi ya kushiriki mfululizo, ikicheza AFCON kwa mara ya 17 mfululizo bila kukosa tangu 1994.

Comoros, Gabon, Sudan na Zimbabwe zimerejea baada ya kukosa AFCON 2023, huku Benin na Uganda zikirejea baada ya kutokuwepo kwa takribani miaka mitano.

Timu nyingine ya kuangaliwa kwa karibu ni Nigeria chini ya kocha raia wa Mali, Eric Chelle, ambao wamefika fainali za AFCON mara 20.

Super Eagles imeshinda AFCON mara tatu: mara ya kwanza mwaka 1980, mara ya pili mwaka 1994 huko Tunisia na taji lao la tatu ililitwaa  2013 Afrika Kusini. 

Msimu huu imepangwa Kundi C pamoja na Tunisia, Uganda na Tanzania inayoshiriki kwa mara ya nne baada ya 1980, 2019 na 2023.

Pia wapo wenyeji Morocco, ambao walishinda AFCON mara ya mwisho 1976 na tangu hapo, mafanikio makubwa zaidi yalikuwa kufika fainali mwaka 2004.

Morocco wamekusanya kikosi kizuri na Kwa mujibu wa Eymael, Atlas Lions chini ya kocha Walid Regragui wana nafasi kubwa kwa sababu wanacheza nyumbani na wana kikosi imara.

“Ni vigumu kuchagua mshindi wa AFCON,” alisema Eymael na kuongeza;

Akizungumza na Flashscore katika mahojiano maalum, kocha Eymael aliyewahi kuinoa Yanga, alipoulizwa ataje timu anayoiona kama mshindi wa AFCON 2025.

 “Lakini nitachagua Morocco kwa sababu wanacheza nyumbani, wana timu yenye ushindani na wana kocha mzuri.”

“Tumeona timu za Morocco za U17, U20 na U23 zikifanya vizuri sana katika miaka ya karibuni na wakati huo huo kuna presha kubwa kwao kushinda AFCON hii.”

“Nimeangalia michezo yao mingi wakati wa hatua za kufuzu na ni timu kamili inayoweza kushindana na kushinda AFCON.”

Akizungumzia mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji hao dhidi ya Comoros, Eymael mwenye umri wa miaka 60, aliyewahi pia kufundisha vilabu kadhaa Afrika ikiwemo AFC Leopards ya Kenyana nyingine za Afrika Kusini,  alikiri kuwa Morocco watakutana na changamoto kubwa lakini mwishowe watashinda.

“Comoros ni timu ngumu kuifunga na kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakijenga timu imara, lakini presha kutoka kwa mashabiki wa Morocco itawasaidia kushinda,” alisema Eymael, ambaye klabu yake ya mwisho ilikuwa Chippa United ya Afrika Kusini.

“Nadhani Morocco watashinda mchezo huu. Ni sawa na Bafana Bafana katika Kombe la Dunia walipocheza dhidi ya Mexico, walishinda kwa msaada wa mashabiki, mchezaji wa 12. Kama wachezaji wa Morocco watahimili presha, nadhani watashinda.”

Eymael aliongeza kuwa:

“Comoros haitakuwa mechi rahisi kabisa; watakuja kuthibitisha kuwa kufuzu kwao AFCON haikuwa bahati.”

Alipoulizwa ni timu ipi inaweza kuizuia Morocco, Eymael alisema:

“Timu inayoweza kuwasumbua Morocco ni DR Congo. Wanapaswa kuwa makini nao, ni timu yenye akili na kocha wao ni mzuri sana kitekniki, lakini bado namba moja kwangu ni Morocco.”

“DR Congo wamekuwa pamoja kwa miaka kadhaa sasa, wana mshikamano mzuri sana. Wanaweza kuwa mshangao mkubwa katika AFCON hii.”

Kuhusu Afrika Kusini, alisema:

“Wameunda kikosi chenye wachezaji kutoka Orlando Pirates, Kaizer Chiefs na Mamelodi Sundowns, wanafahamiana vizuri, wana mshikamano mzuri, watakuwa na AFCON nzuri, lakini sidhani kama watafikia kiwango walichokionyesha AFCON iliyopita.”

Eymael alihitimisha kwa kusema:

“Watu wengi wataizungumza Senegal, wataizungumza Nigeria, lakini sidhani kama Nigeria wataweza kurudia mafanikio ya AFCON iliyopita.”

Baada ya kucheza na Comoros katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah kesho Jumapili kuanzia saa 4:00, Morocco waliopo Kundi A, watacheza dhidi ya Mali kabla ya kumalizia kwa Zambia.