Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya usajili yamtafuna Mikel Arteta

Mikel Pict
Mikel Pict

Muktasari:

  • Katika mahojiano yake Arteta alisema uamuzi wa kutosajili haikuwa kamari licha Gabriel Jesus na Bukayo Saka kuwa na majeraha kwa wakati huo, kabla ya wiki hii kupata pigo lingine la kuumia kwa Kai Havertz.

LIVERPOOL, ENGLAND: SAA kadhaa baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili la Januari, Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alijitetea vikali kuhusu hali ya timu yake kutosajili mchezaji yeyote wa kuongeza nguvu katika safu yao ya ushambuliaji iliyokuwa inawakosa mastaa wake muhimu.

Katika mahojiano yake Arteta alisema uamuzi wa kutosajili haikuwa kamari licha Gabriel Jesus na Bukayo Saka kuwa na majeraha kwa wakati huo, kabla ya wiki hii kupata pigo lingine la kuumia kwa Kai Havertz.

Wakati huo, kocha huyu Mhispania aliulizwa ikiwa ataendelea kumtumia Havertz peke yake kwa muda wote kama mshambuliaji wa kati kipindi Jesus na Saka wakiwa nje kwa majeraha alisema inawezekana staa huyo kucheza kwa kipindi chote na akamsifia ana nguvu ya kiasili.

Ilipofika Februari 4, mwaka huu Arteta aliulizwa tena juu ya mwenendo wa timu yake ikiwa anajuta kutokufanya usajili na alisema: “Tuna masikitiko, lakini tunapaswa kuendelea. Hakuna anayejua kama tungepata faida kwa kusajili au tungepata hasara. Tutajua mwishoni mwa msimu.”

Siku nane baada ya mkutano huo, Arteta tayari amepata jibu kwa asilimia nyingi uamuzi wa kutosajili ulikuwa ni mbaya baada ya kuumia kwa Havertz pia.

Havertz alipata majeraha ya misuli ya paja wakati wa mazoezi kwenye kambi ya timu hiyo huko Dubai wiki hii na jeraha alilopata linadaiwa litamweka nje hadi mwisho wa msimu.

Kuumia kwake kunamweka katika hali mbaya Arteta atakayelazimika kutumia chaguo lake la tatu eneo la mshambuliaji wa kati na kwa sasa ni  Leandro Trossard ambaye kiasili ni winga pamoja na  Ethan Nwaneri mwenye umri wa miaka 17  ambaye amezoeleka zaidi kama kiungo mshambuliaji ingawa anaweza pia kucheza kama mshambuliaji wa kati.

Staa mwingine ambaye Arteta anaweza kumtumia ni Raheem Sterling lakini haonekani kuwa na imani naye sana kwani hamchezeshi mara kwa mara.

Mbali ya Havertz, Arteta pia anaikosa huduma ya Gabriel Martinelli anayetarajiwa kukaa nje walau mwezi mmoja kutokana na majeraha ya misuli ya paja na huyu pia angeweza kucheza eneo hilo la mshambuliaji wa kati.

Hii itamfanya Arteta kuiongoza Arsenal kwa miezi miwili bila yakuwa na washambuliaji wake tegemeo kwani Martinelli na Saka wanatarajiwa kurejea Machi, lakini itakuwa ngumu kuwaingiza moja kwa moja kwa sababu wanaweza kupata majeraha tena.

Hata hivyo, lawama kubwa huenda zikamwangukia  mkurugenzi wa michezo wa muda wa washika mitutu hao, Jason Ayto, kwa  kushindwa kwake katika majadiliano ya kushusha washambuliaji waliohitajika kwenye dirisha  lililopita.

Ayto ambaye alichukua mikona ya Edu aliyejiuzuru kutoka nafasi yake Novemba mwaka jana analaumiwa kwa kushindwa kuwa na uharaka wa kukamilisha usajili wa mastaa waliopendekezwa na Arteta Januari.

Katika wachezaji watatu waliopo kwa sasa ambao Arteta anaweza kuwatumia kama washambuliaji wa kati au namba tisa,  Trossard na Sterling wamewahi kucheza kama tisa wa uongo hapo kabla, hivyo kocha anaweza kuendeleza mgumo wake wa kawaida wa  4-3-3.

Nwaneri pia anaweza kupangwa katika nafasi hiyo, baada ya kufunga mabao matatu katika mashindano yote mwaka 2025, huku Arteta akiwahi kusema hiyo ni nafasi ambayo kijana huyo anaweza kuicheza baadaye katika maisha yake ya soka.