Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ILE SIKU NDO LEO! Afcon 2025 kinawaka, Morocco v Comoros utamu uko hapa

Muktasari:

  • Morocco ambao ni wenyeji wa mashindano hayo ya 35 yanayofahamika kama Afcon 2025 watashuka uwanjani Prince Moulay Abdellah huko Rabat kurusha kete yao ya kwanza wakati itakapokipiga na Komoros.

RABAT, MOROCCO: HAYAWI hayawi yamekuwa. Baada ya kungoja kwa miaka, miezi, wiki na sasa ile siku imewadia na utepe wa mashindano ya kusaka ubingwa wa Afrika utakatwa huko Morocco usiku wa leo Jumapili.

Morocco ambao ni wenyeji wa mashindano hayo ya 35 yanayofahamika kama Afcon 2025 watashuka uwanjani Prince Moulay Abdellah huko Rabat kurusha kete yao ya kwanza wakati itakapokipiga na Komoros.

Mechi hiyo ya ufunguzi inasubiriwa na mashabiki wengi wa soka la Afrika ili kuanza kuona uhondo unaotarajiwa kwenye mikikimikiki hiyo ya mashindano ya Afcon 2025.

Morocco inashika nafasi ya 11 kwenye viwango vya soka vya dunia, huku ikishika namba moja kwa Afrika, wakati Comoros yenyewe inashika nafasi ya 108.

Timu hizo mbili zimewahi kukutana mara nne na Morocco ilishinda tatu na moja ilimalizika kwa sare. Mechi yao ya kwanza ilikuwa ya kufuzu Afcon 2019, kwenye Kundi C na Morocco ikishinda 1–0, Oktoba 13, 2018, wakati mechi ya pili ilichezwa Comoros, siku tatu baadaye na kumalizika kwa sare ya mabao 2–2. Morocco ilifuzu ikiwa vinara wa kundi sambamba na Cameroon na hivyo kwenda Afcon 2019, iliyofanyika Misri.

Zilipokutana Januari 14, 2022 kwenye mechi ya Kundi C ya michuano ya Afcon 2021, Morocco ilishinda 2–0 huko Yaoundé, Cameroon shukrani kwa mabao ya Selim Amallah na Zakaria Aboukhlal. Na sasa miamba hiyo itakutana kwenye ufunguzi wa mikikimikiki ya Afcon 2025. Itakuwaje?

Mechi hiyo itakuwa ya Kundi A, huku Comoros ikipata bahati ya kucheza dhidi ya timu mwenyeji kwa mara ya pili mfululizo katika mashindano ya Afcon. Kwenye fainali zilizopita, walichapwa 2-1 na Cameroon, Januari 24, 2022 katika kipute cha Raundi ya 16 bora kwenye Afcon 2021. Kwenye Afcon 2021, Morocco na Comoros zilipangwa kwenye Kundi C na zote zilifuka hatua ya makundi na Comoros ilifanya hivyo kwa tiketi ya timu namba tatu bora kwenye kundi lililokuwa pia na timu za Gabon iliyomaliza namba mbili na Ghana namba nne.

Lakini, safari hii timu hizo zitafungua kwenye Afcon 2025, ambazo ni fainali za 35, huku zile 34 zilizopita, mechi zake za ufunguzi ni moja tu, ndiyo iliyomalizika kwa 0-0, Afrika Kusini dhidi ya Cabo Verde, 2013. Hiyo ina maana, mechi za ufunguzi za Afcon mara nyingi zimekuwa za mabao.

Morocco imetajwa wachezaji wake bora kabisa kwenye kikosi, sawa na ilivyo kwa Comoros na kufanya mechi hiyo kutabiriwa kuwa na mvuto mkubwa kwa mashabiki. Nani atapigwa ni suala la kungoja na kuona.

Morocco imepania kuweka rekodi ya kuwa mwenyeji na kushinda ubingwa na timu ya mwisho mwenyeji kunyakua taji kwenye Afcon ilikuwa Ivory Coast kwenye Afcon iliyopita na yenyewe ilikuwa ya kwanza tangu Misri ibebe 2006.

Kitu kingine ni kwamba mwenyeji au mwenyeji mwenza hajawahi kupoteza mechi ya kwanza katika Afcon 15 zilizopita. Timu ya mwisho iliyokuwa mwenyeji kupoteza mechi ya ufunguzi ilikuwa Burkina Faso mwaka 1998, ilipochapwa 1–0 na Cameroon. Katika karne ya 21 hakuna timu mwenyeji iliyopoteza mechi ya ufunguzi na ushindi ni mara tisa na sare sita.

Kwenye siku ya ufunguzi ya mashindano ya Afcon 2025 itapigwa mechi hiyo moja tu, lakini siku inayofuatia, Jumatatu zitapigwa mechi tatu za kibabe kabisa. Kivumbi cha siku hiyo kitashuhudiwa kwa mechi jioni kati ya Mali na Zambia, kabla ya usiku kuzishuhudia Afrika Kusini ikipepetana na Angola, wakati Misri itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Zimbabwe.

Jumanne kutakuwa na mechi nne, lakini ile inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka hapa nchini, itakuwa usiku baina ya Nigeria na Taifa Stars ya Tanzania. Mambo ni moto.

Vikosi vinavyotarajiwa

Morocco: Bono; Mazraoui, Aguerd, El Yamiq, Salah-Eddine; Ben Seghir, El Aynaoui, Saibari; Diaz, En-Nesyri, Ezzalzouli

Comoros: Anzimati-Aboudou; B. Youssouf, M’Dahoma, Soilihi, Toibibou, Boura; M’Changama, Z. Youssouf, Bourhane; Said, Selemani.