Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi hapa sheria mpya zilizoongezwa EPL

Muktasari:

  • Vinginevyo marefa watakaokuwa kwenye vyumba vya VAR hawatoruhusiwa kuingilia maamuzi ya marefa wa uwanjani kama hawajawa na uhakika wa moja kwa moja kuhusu kosa lililofanywa na anayechezesha mechi.

London. Msimu wa Ligi Kuu ya England (EPL) umeanza na mabadiliko ya vipengelee kadhaa katika sheria za soka ambayo yanategemewa kuongeza mvuto wa ligi hiyo.

Miongoni mwa mabadiliko yaliyofanyika ni refa msaidizi wa teknolojia ya video ya usaidizi kwa waamuzi (VAR) kuingilia tukio pale tu atajiridhisha kwamba mwamuzi wa uwanjani amefanya kosa la wazi.

Vinginevyo marefa watakaokuwa kwenye vyumba vya VAR hawatoruhusiwa kuingilia maamuzi ya marefa wa uwanjani kama hawajawa na uhakika wa moja kwa moja kuhusu kosa lililofanywa na anayechezesha mechi.

Lengo la hilo ni kupunguza usimamishaji wa mara kwa mara wa mchezo ambao umekuwa ukilalamikiwa kuwa unaondoa mvuto wa mechi lakini pia kusababisha mchezo kuchezwa kwa muda mrefu.

"Tunatakiwa kujiamini na kutochunguza kwa undani sana katika tathmini yetu," alisema kiongozi wa kamati ya waamuzi wa soka England (PGMOL), Howard Webb.

Pia mashabiki wa soka watapata fursa ya kufafanuliwa kuhusu maamuzi mbalimbali yaliyotokana na VAR kupitia ukurasa maalumu wa mtandao wa X wa EPL lakini pia kupitia luninga kubwa ambazo zimefungwa viwanjani.

Ni msimu ambao unaweza kushuhudiwa kutokuwa na idadi kubwa ya dakika za nyongeza kama ilivyokuwa msimu uliopita kutokana na marekebisho ya sheria ya muda yaliyofanywa ili kudhibiti ushangiliaji bao kwa muda mrefu.

Kwa sasa muda huongezwa kwa kila sekunde kati ya pale mpira unapoingia nyavuni na unapoanzishwa katikati mwa uwanja.

Katika mabadiliko mapya, muda utaanza kuhesabiwa sekunde 30 baada ya bao kufungwa hivyo mchezo utakaokuwa na mabao sita, utakuwa na dakika za nyongeza zisizozidi tatu.

Mabadiliko mengine ni kuanza kutolewa kwa adhabu kwa wachezaji wa timu inayopiga mkwaju wa faulo ambao watakuwa wanasimama mbele ya ukuta uliopangwa na wachezaji wa timu pinzani kwa lengo la kuwakinga wasiuone mpira kirahisi unapoelekezwa langoni mwao.

Sheria ya mkono kufuata mpira italegezwa kidogo. Wachezaji sasa hawalazimiki kusogea huku mikono yao ikiwa imefichwa pembeni au nyuma ya migongo yao.

Msimamo wa mkono au mkono wao utahukumiwa kuhusiana na mjongeo wa mwili.

"Tunapata hisia kwamba tunatoa mipira mingi ya adhabu za mikono kufuata mpira kwa vitendo ambavyo ni vya kawaida kabisa na vinavyokubalika.

"Mwongozo kwa viongozi msimu huu ni mdogo ni zaidi. Utaona penalti chache za mpira wa mikono," alisema Webb.

Wakati huohuo, mpira unaogusa mikono usio wa makusudi unaoongoza kwenye adhabu hautakuwa tena kosa la kuweka nafasi moja kwa moja.

Pia mabadiliko mengine yatashuhudiwa wakati wa pigo la penalti mpira lazima uwe juu au katikati ya alama ya kuwekea mpira na sio kwingineko.