Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hawa hapa watupiaji wa Klabu Bingwa Dunia

Muktasari:

  •  Mashindano hayo yataanza Juni 14 na kuhitimishwa Julai 13 yakichezewa katika viwanja 12 nchini humo.

MIAMI, MAREKANI: MWEZI ujao, macho ya ulimwengu wa soka yatageukia Marekani ambako kutafanyika mashindano ya Kombe la Dunia la Klabu ambapo utakuwa ni muundo mpya utakaohusisha timu  32 bora kutoka mabara yote.

 Mashindano hayo yataanza Juni 14 na kuhitimishwa Julai 13 yakichezewa katika viwanja 12 nchini humo.

Bingwa mtetezi wa taji hilo, Manchester City ya England iliyotwaa ubingwa  2023 baada ya kuichapa Fluminense ya Brazil kwa mabao 4-0 kwenye fainali iliyopigwa jijini Jeddah, Saudi Arabia, ni miongoni mwa timu shiriki kutoka England ikiwa ni pamoja na Chelsea.

Hapa tunatazama mastaa ambao wanaongoza hadi sasa kwa kufunga mabao mengi zaidi katika michuano hiyo mara kadhaa walizocheza.


SALEM AL-DAWSARI (4) - AL-HILAL

Salem Al-Dawsari alikuwa miongoni mwa majina maarufu zaidi katika Ligi Kuu  Saudi Arabia kabla ya mastaa wa Ulaya kuanza kutua nchini humo.

Winga huyo ameshiriki Kombe la Dunia la Klabu mara tatu akifunga mabao manne katika kipindi hicho. Katika mashindano ya 2019/20 aliisaidia Al-Hilal kufika hatua ya mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu, lakini walipoteza kwa penalti dhidi ya Flamengo.

Aliisaidia tena Al Hilal  miaka miwili baadaye kufika hatua ya nusu fainali ambapo ilipoteza mbele ya Chelsea kisha ikapoteza kwa Al Ahly katika mchezo wa mshindi wa tatu. Katika michuano yote aliyoshiriki staa huyo alifunga mabao manne.


PEDRO (4) -Flamengo

Pedro alitarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji bora wa Brazil waliotabiriwa kwamba wangeenda  kung’ara Ulaya, hata hivyo mambo hayakwenda kama ilivyotarajiwa licha ya kusajiliwa na Fiorentina.

Ni kama staa huyo iliandikwa atang’ara akiwa Amerika Kusini tu kwani alionyesha kiwango bora akiwa na Flamengo, ambako alikuwa na wastani wa kufunga bao kwenye kila mechi mbili.

Hilo lilidhihirika katika Kombe la Dunia la Klabu 2022/23 ambapo akiwa na umri wa miaka 27 alifunga mabao manne katika mechi mbili kuisaidia timu yake kumaliza nafasi ya tatu.

 Mabao yake mawili ya mwisho dhidi ya Al Ahly yaliwafanya watoke nyuma kwa matokeo ya 2-1 na kushinda 4-2.


CESAR DELGADO (5)-Monterrey

Katika maisha yake ya soka Cesar Delgado alichezea timu kadhaa ikiwemo Cruz Azul, Olympique Lyonnais na Atlas. Hata hivyo alishiriki Kombe la Dunia la Klabu akiwa na Monterrey ya Mexico. Aliiwakilisha timu hiyo kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2012 hadi 2014 akifunga mabao matano.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alikuwa mhimili wa mashambulizi ya timu, akicheza kama winga au kiungo wa kati.


LIONEL MESSI (5) Barcelona

Lionel Messi hahitaji utambulisho. Ni mmoja wa wachezaji bora zaidi wa muda wote. Kutokana na kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu, Messi alishiriki Kombe la Dunia la Klabu mara tatu.

Katika mashindano ya 2009 na 2011, Messi alishinda tuzo ya mfungaji bora ambapo mara zote hizo Barca ilikuwa bingwa.

Mwaka 2015 alimaliza wa pili nyuma ya Luis Suarez katika suala la utupiaji.


LUIS SUAREZ (5) Barcelona

Luis Suarez ni mmoja wa wachezaji bora kuwahi kutokea katika kikosi cha Barcelona. Ushirikiano wake na Messi pamoja na Neymar ulikuwa wa kuvutia na uliisaidia Barca kushinda mataji mbalimbali kama Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus mwaka 2015.

 Miezi michache baadaye walishiriki Kombe la Dunia la Klabu  na nyota huyo wa zamani wa Liverpool alionyesha makali kwa kufunga hat-trick katika nusu fainali dhidi ya Guangzhou kisha akafunga mabao mawili ya mwisho kwenye fainali dhidi ya River Plate iliyomalizika kwa Barca kushinda 3-0.

Hizo ndizo mechi mbili pekee alizocheza katika mashindano hayo, lakini aliweza kufunga mabao matano — na akashinda tuzo ya mfungaji bora kwa mwaka huo.


KARIM BENZEMA (6)- Real Madrid/ Al Ittihad

Unapozungumzia kuhusu washambuliaji bora wa muda wote jina la Karim Benzema huwezi kuliacha. Alifunga bao muhimu katika fainali ya 2016 dhidi ya Kashima Antlers na kuiwezesha Madrid kushinda michuano ya mwaka huo.

Mshambuliaji huyo wa Ufaransa alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika fainali nne  tofauti za michuano ya Kombe la Dunia la Klabu 2023 baada ya kufunga dhidi ya Auckland City akiwa na Al-Ittihad.


GARETH BALE (6)- Real Madrid

Gareth Bale alistaafu 2023, akiacha historia ya kipekee kutokana na rekodi zake katika michuano mbalimbali.

Bale ambaye alijiunga na Real Madrid 2013 alikuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo  kilichoshinda mashindano ya Kombe la Dunia la Klabu  2014, 2016 na 2017, huku akifunga mabao muhimu na kutoa asisti kadhaa za mabao.

Alifunga bao la pili dhidi ya San Lorenzo kwenye fainali ya 2014 na pia katika mashindano ya 2018, alishinda tuzo ya mfungaji bora baada ya kufunga mabao matatu.


CRISTIANO RONALDO (7)- Real Madrid/Manchester United

Cristiano Ronaldo ambaye anatajwa kuwa mchezaji bora wa Ureno wa muda wote. Pia ndiye mshambuliaji mwenye mabao mengi zaidi katika michuano hiyo.

Ronaldo ambaye hadi sasa amezichezea timu tano za Sporting Lisbon, Manchester United, Real Madrid, Juventus na Al-Nassr ameshiriki michuano hiyo akiwa na timu mbili tu. Kwanza ilikuwa ni Man United ambapo baada ya kuchukua Ligi ya Mabingwa 2008 walikwenda kucheza michuano ya Klabu Bingwa Dunia na kufanikiwa kushinda pia wakati huo akifunga bao katika nusu fainali dhidi ya Gamba Osaka.

Akiwa na Real Madrid, mchezaji huyo alikwenda kushinda taji hilo mara tatu na katika misimu miwili alifanikiwa kumaliza kama mfungaji bora wa mashindano.