Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harry Kane: Levy?  Hii sio poa

KANE Pict

Muktasari:

  • Taarifa za mapema wiki hii zilibainisha Levy ameng'atuka kwenye kikosi hicho cha Spurs baada ya kuwa mwenyekiti kwa kipindi cha miaka 25. Bosi huyo ameondolewa kwenye timu na wamiliki wenye hisa nyingi kwenye kikosi hicho, familia ya Lewis.

MUNICH, UJERUMANI: STRAIKA, Harry Kane amesifu kazi bora kabisa iliyofanywa na Daniel Levy kwenye kikosi cha Tottenham Hotspur baada ya bosi huyo kung'oka kwenye kikosi hicho cha London.

Taarifa za mapema wiki hii zilibainisha Levy ameng'atuka kwenye kikosi hicho cha Spurs baada ya kuwa mwenyekiti kwa kipindi cha miaka 25. Bosi huyo ameondolewa kwenye timu na wamiliki wenye hisa nyingi kwenye kikosi hicho, familia ya Lewis.

Levy ameamua kuachana na Spurs baada ya miongo miwili na nusu na alijitengenezea umaarufu kama mmoja wa mabosi wagumu sana kwenye kufanya naye mazungumzo ya kusajili mchezaji kwenye timu hiyo. Moja ya wachezaji waliowahi kugomewa na Levy wasiondoke ni Kane, ambaye mwaka 2023 alikwenda kujiunga na Bayern Munich kwa pesa ndefu.

“Ukweli ni kitu kilichonishangaza, kama nitaamua kusema ukweli,” alisema Kane.

“Sikutarahia, sikuona hilo likitokea. Daniel amekuwa mwenyekiti mahiri kabisa kwenye klabu ya Tottenham, zaidi ya miaka 20 akiwa hapo. Kwa kuzingatia klabu ilipofika na ilipo kwa sasa, kuna mabadiliko makubwa sana, si tu uwanjani hadi nje pia."

Levy amefanya mambo makubwa katika kuibadilisha Spurs kuwa timu shindani kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England kwa miaka ya karibuni, lakini familia ya mmiliki, Lewis imeamua kumfungulia mlango wa kutokea na kufanya mambo tofauti.

Licha ya kwamba mashabiki kuna wakati waliandamana kumpinga Levy, lakini kuondoka kwake kimekuwa kitu cha mshtuko mkubwa kwa straika Kane na kukiri kwamba si kitu kinachoingia akili kuona bosi huyo akiondoka kwenye kikosi hicho.