Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Garnacho, Napoli kuna kitu

GERNACHO Pict
GERNACHO Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa Man United ipo tayari kumuuza staa huyu lakini inahitaji kiasi cha pesa kisichopungua Pauni 40 milioni ili kumuacha aende.

MKURUGENZIwa michezo wa Napoli, Giovanni Manna anatarajia kukutana na wawakilishi wa Manchester United kujadili uwezekano wa kuipata saini ya winga wa timu hiyo na Argentina, Alejandro Garnacho, 22, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa Man United ipo tayari kumuuza staa huyu lakini inahitaji kiasi cha pesa kisichopungua Pauni 40 milioni ili kumuacha aende.

Awali, baada ya Ruben Amorim kupewa mikoba ya kuinoa Man United, miongoni mwa wachezaji ambao hawakuwa wanapata nafasi ya kucheza ni Garnacho na moja kati ya sababu ambazo kocha huyo alizieleza kuwa zinasababisha asimpe sana nafasi ni kutofanya vile ambavyo yeye anahitaji.

Garnacho alikuwa katika kundi moja na Marcus Rashford ambaye alilazimika kuondoka kwa mkopo Januari baada ya kuona pia hana nafasi.

Garnacho amezungumzwa sana baada ya kuhoji kutoanzishwa katika mechi ya fainali ya Europa League ambayo Man United ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Tottenham.

Mkataba wa sasa wa  Garnacho unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu huu amecheza mechi 58 za michuano yote na kufunga mabao 11.


Kaoru Mitoma

ARSENAL imejumuika pamoja na Bayern Munich katika mbio za kuiwania saini ya kiungo wa kati wa Brighton na timu ya taifa ya Japan mwenye umri wa miaka 28, Kaoru Mitoma katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mitoma ambaye katika dirisha lililopita pia alikuwa akihitajika na vigogo wa Saudi Arabia, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Viktor Gyokeres

MSHAMBULIAJI wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Sweden, Viktor Gyokeres anatarajiwa kuaondoka kwenye timu hiyo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo huenda akatimkia  Arsenal au Chelsea ambazo zote zinafanya mazungumzo na wawakilishi wake.

Awali, fundi huyu alihusishwa na timu nyingi lakini baadhi zimeonekana kujiondoa na hadi sasa zimebakia hizo mbili.


Emiliano Martinez

ARSENAL inataka kumsajili kipa wa Aston Villa na Argentina, Emiliano Martinez, mwenye umri wa miaka 32, katika dirisha lijalo baada ya kipa wao Mhispania, David Raya kuripotiwa kwamba yupo kwenye rada za Real Madrid inayotaka kumsajili katika dirisha hili. Mkataba wa Emiliano unamalizika mwaka 2029, hivi karibuni vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya vilitangaza kwamba fundi huyu ataondoka baada ya msimu kumalizika. Alitokea Arsenal.


Kevin de Bruyne

RAIS wa Napoli, Aurelio de Laurentiis amethibitisha kuwa timu hiyo inafanya mazungumzo na kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne na imedhamiria kumsajili katika dirisha lijalo.

Ripoti zinaeleza, Napoli inataka kumpa kiungo huyu mkataba wa miaka mitatu ambao utamwezesha kuvuna Pauni 23 milioni kwa miaka yote hiyo ambazo ni sawa na Pauni 159,722 kila wiki.


Rafael Leao

MKURUGENZI wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta amefanya mazungumzo na winga wa AC Milan, Rafael Leao, mwenye umri wa miaka 25, katika jitihada za kumshawishi ajiunge nayo katika dirisha lijalo. Hata hivyo, inaonekana kuwa ngumu kumshawishi fundi huyu kwa sababu pia anadaiwa kuwa na ofa kutoka kwa vigogo wengine wa Ulaya ikiwamo Real Madrid.


Benjamin Sesko

ARSENAL imewasilisha ofa kwenda  RB Leipzig kwa ajili ya kumsajili  mshambuliaji wa timu hiyo mwenye umri wa miaka 21, Benjamin Sesko, katika dirisha lijalo. Sesko ni mmoja kati ya washambuliaji walioonyesha kiwango bora katika michuano ya Bundesliga kwa msimu uliomalizika ambapo alicheza mechi 45 za michuano yote na kufunga mabao 21.


Matheus Fernandes

ASTON Villa, West Ham na Leeds zinamfuatilia kiungo wa Southampton na timu ya taifa ya Ureno chini ya miaka 21, Matheus Fernandes, mwenye umri wa miaka 20.

Fernandes ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, msimu huu amecheza mechi 43 za michuano yote na kufunga mabao matatu.