Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fahamu haya Kombe la dunia la klabu linavyonukia kuanza

FIFA Pict

Muktasari:

  • Michuano hiyo inayotarajiwa kuanza mwezi ujao itafanyika huko Marekani na itamalizika Julai 13 itakuwa ni mapinduzi makubwa kuanzia kiuchumi na maeneo mengine.

FLORIDA, MAREKANI: MWAKA huu  historia mpya inaandikwa katika ulimwengu wa soka kwa kufanyika michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa klabu ambayo itakuwa kwa mfumo mpya ikihusisha jumla ya timu 32 kutoka mabara tofauti.

Michuano hiyo inayotarajiwa kuanza mwezi ujao itafanyika huko Marekani na itamalizika Julai 13 itakuwa ni mapinduzi makubwa kuanzia kiuchumi na maeneo mengine.

Hapa tumekuletea baadhi ya mambo muhimu ya kufahamu wakati michuano hii ambayo hapo awali ilikuwa ikishirikisha timu saba ikikaribia kuanza.


1. Mfumo Mpya wa Mashindano

Kwa mara ya kwanza, mashindano haya yatafuata mfumo wa makundi, mtoano, robo fainali hadi fainali, kama ilivyo kwenye michuano mikubwa ya kimataifa.

Timu 32 zitagawanywa katika makundi manane ya timu nne-nne.

Timu mbili bora kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya mtoano (16 bora)

Kutakuwa na mechi ya mchujo ya kutafuta mshindi  wa tatu , nusu fainali, na fainali

Mfumo huu unakusudia kuongeza mvuto, ushindani, na fursa kwa mashabiki kushuhudia timu kutoka mabara tofauti vikikabiliana.


2. Mgawanyo wa Vilabu kwa Bara

FIFA ilitumia vigezo vya mafanikio ya klabu katika mashindano ya mabara yao kuanzia 2021 hadi 2024 ili kuamua timu zitakazoshiriki.

Ulaya (UEFA) – 12

Amerika Kusini (CONMEBOL) – 6

Afrika (CAF) – 4

Asia (AFC) – 4

Amerika Kaskazini, Kati na Karibiani (CONCACAF) – 4

Oceania (OFC) – 1

Mwenyeji (USA) – 1

Baadhi ya vilabu vilivyothibitishwa kushiriki ni Real Madrid, Manchester City, Chelsea, Bayern Munich, Flamengo, Al Ahly, na Wydad Casablanca.

FIFA 01

3. Zawadi nono

Michuano hii imekuwa kivutio kikubwa si kwa umaarufu tu, bali pia kwa thamani yake ya kifedha. FIFA imetangaza zawadi ya jumla ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 1 (zaidi ya trilioni moja kwa pesa za Tanzania).

Zawadi hiyo imegawanywa katika sehemu kuu mbili, eneo la kwanza ni kiwango cha uwanjani ambapo imetengwa Dola 475 milioni.

Kila timu itakaposhinda  mechi ya makundi itapata Dola 2 milioni, Sare ya makundi ni Dola 1 milioni, 16 bora ni Dola 7.5 milioni, kufuzu robo fainali, dola 13.125 milioni, nusu dola 21 milioni, mshindi wa pili – Dola 30 milioni na bingwa ni Dola 40 milioni.

Pesa za zawadi pia zitatolewa kwa timu shiriki ambapo imetengwa jumla ya dola 525 milioni. Timu zote zitapokea malipo ya awali kwa kushiriki, kulingana na bara na viwango vya mafanikio.

Timu kutoka Ulaya zitakunja Dola 38 milioni kila mmoja kwa ushiriki wao wakati zile za Afrika na Asia zikikunja dola 9.5 milioni, huku upande wa timu kutoka  Oceania zikipata dola 3.5 milioni.

Vilevile limetengwa fungu la Dola 250 milioni kwa ajili ya kusaidia timu ndogo za  barani Afrika, Asia, na Amerika ya Kati. Hii inalenga kukuza maendeleo ya soka duniani kote.


MAMBO YA KUFAHAMU

-Katika hatua ya makundi, vilabu kutoka nchi au bara moja (kama EPL, La Liga n.k.) havitaruhusiwa kuwa kundi moja, ili kuhakikisha utofauti wa ushindani.


-Katika hatua ya mtoano, hakutakuwa na muda wa ziada (extra time) hadi nusu fainali. Mechi zitaamuliwa kwa penalti moja kwa moja ikiwa sare.


-FIFA italipa gharama zote kuu za timu zote ikiwemo hoteli, ndege za kimataifa, usafiri wa ndani, chakula, na kambi za mazoezi.


-FIFA inatarajia zaidi ya mashabiki milioni 2 kuhudhuria moja kwa moja

Kwa mashabiki wa Marekani na kutoka nje, FIFA inakadiria kuhudumia zaidi ya watu milioni 2 kwenye viwanja tofauti.

FIFA 02

Timu mbili bora kutoka kila kundi zitafuzu hatua ya mtoano (16 bora).

Kutakuwa na mechi ya mchujo ya kutafuta mshindi wa tatu, nusu fainali, na fainali.

Mfumo huu unakusudia kuongeza mvuto, ushindani na fursa kwa mashabiki kushuhudia timu kutoka mabara tofauti zikikabiliana.


2. Mgawanyo wa klabu kwa Bara

FIFA ilitumia vigezo vya mafanikio ya klabu katika mashindano ya mabara yao kuanzia 2021 hadi 2024 ili kuamua timu zitakazoshiriki.

Ulaya (UEFA) – 12

Amerika Kusini (CONMEBOL) – 6

Afrika (CAF) – 4

Asia (AFC) – 4

Amerika Kaskazini, Kati na Karibiani (CONCACAF) – 4

Oceania (OFC) – 1

Mwenyeji (USA) – 1

Baadhi ya klabu zilizothibitishwa kushiriki ni Real Madrid, Manchester City, Chelsea, Bayern Munich, Flamengo, Al Ahly, na Wydad Casablanca.


3. Zawadi nono

Michuano hii imekuwa kivutio kikubwa si kwa umaarufu tu, bali pia kwa thamani yake ya kifedha. FIFA imetangaza zawadi ya jumla ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 1 (zaidi ya Sh 2.6 trilioni kwa pesa za Tanzania).

Zawadi hiyo imegawanywa katika sehemu kuu mbili, eneo la kwanza ni kiwango cha uwanjani ambapo imetengwa Dola 475 milioni.

Kila timu itakaposhinda  mechi ya makundi itapata Dola 2 milioni, sare ya makundi ni Dola 1 milioni, 16 bora ni Dola 7.5 milioni, kufuzu robo fainali, dola 13.125 milioni, nusu dola 21 milioni, mshindi wa pili – Dola 30 milioni na bingwa ni Dola 40 milioni.

Pesa za zawadi pia zitatolewa kwa timu shiriki ambapo imetengwa jumla ya Dola 525 milioni. Timu zote zitapokea malipo ya awali kwa kushiriki, kulingana na bara na viwango vya mafanikio.

Timu kutoka Ulaya zitakunja Dola 38 milioni kila mmoja kwa ushiriki wao wakati zile za Afrika na Asia zikikunja Dola 9.5 milioni, huku upande wa timu kutoka Oceania zikipata dola 3.5 milioni.

Vilevile limetengwa fungu la Dola 250 milioni kwa ajili ya kusaidia timu ndogo za barani Afrika, Asia, na Amerika ya Kati. Hii inalenga kukuza maendeleo ya soka duniani kote.


MAMBO YA KUFAHAMU

-Katika hatua ya makundi, klabu kutoka nchi au bara moja (kama EPL, La Liga n.k.) hazitaruhusiwa kuwa kundi moja, ili kuhakikisha utofauti wa ushindani.

-Katika hatua ya mtoano, hakutakuwa na muda wa ziada (extra time) hadi nusu fainali. Mechi zitaamuliwa kwa penalti moja kwa moja ikiwa sare.

-FIFA italipa gharama zote kuu za timu zote zikiwamo za malazi katika hoteli zitakazofikia, ndege za kimataifa, usafiri wa ndani, chakula, na kambi za mazoezi.

-FIFA inatarajia zaidi ya mashabiki milioni 2 kuhudhuria moja kwa moja.

Kwa mashabiki wa Marekani na kutoka nje, FIFA inakadiria kuhudumia zaidi ya watu milioni 2 kwenye viwanja tofauti.