Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

England yatumia wake,wapenzi kuwapa wachezaji utulivu Marekani

Muktasari:

  • Wanawake hao wamepelekwa huko ili wachezaji wa England waweze kupumzika nao wasipokuwa bize na ishu za mechi katika Jiji la Florida kwenye mji ambao nyuzi joto inadikia 34°C na unyevunyevu unaofikia asilimia 80 unaowapa shida watu mitaani wanapotembea.

WAKE na wapenzi wa wachezaji wa timu ya taifa ya England tayari wameshawasili Marekani wakiwa na 'mahasibandi na maboifredi' wao kwa ajili ya kuwapa kampani katika michuano ya Kombe la Dunia 2026 inayoanza kesho.

Wanawake hao wamepelekwa huko ili wachezaji wa England waweze kupumzika nao wasipokuwa bize na ishu za mechi katika Jiji la Florida kwenye mji ambao nyuzi joto inadikia 34°C na unyevunyevu unaofikia asilimia 80 unaowapa shida watu mitaani wanapotembea.

Hata hivyo, kocha wa timu hiyo, Thomas Tuchel amefichua kuwa wenza wa wachezaji hao wanaungana nao mapema kabla ya mashindano kuanza, kinyume na utaratibu wa kawaida.

Alisema: “Tutakuwa nao Marekani mapema sana, mapema kuliko timu nyingine pengine. Tutakuwa nao kujiandaa na joto na unyevunyevu.

Tutakuwa na kambi ya mapema itakayoruhusu mchanganyiko mzuri kati ya muda wa mapumziko, muda wa familia na marafiki, na mpira wa miguu.”

Mchumba wa Bukayo Saka, Tolami Benson, na mpenzi wa Jude Bellingham, Ashlyn Castro, wanatarajiwa kuwepo pamoja na mke wa Ollie Watkins, Ellie. Wageni wengine wanaoweza kuwepo ni pamoja na mpenzi wa Kobbie Mainoo, Layla Roye, na mke wa John Stones, Olivia.

Ni jambo lisilo la kawaida kwa wenza wa wachezaji wa England kuungana nao katika nchi mwenyeji wa Kombe la Dunia kabla ya mashindano kuanza. Watakuwa Marekani kwa mikusanyiko ya kawaida baada ya mazoezi huku wachezaji na makocha pekee wakiruhusiwa katika hoteli ya timu.

Pia inatarajiwa kuwa watakuwa wakimya zaidi kuliko mashindano ya Kombe la Dunia Ujerumani 2006, ambapo wake wa mastaa wa nchi hiyo walionekana mitaani wakijimwaya na kujiachia sambamba na walinzi wao.

Wataalamu wanasema mashindano hayo yatakayofanyika Marekani, Mexico na Canada, kuanzia leo yatakuwa Kombe la Dunia lenye joto kali zaidi kuwahi kutokea na wameionya Fifa kuhusu hatari kwa wachezaji, ambapo watakuwa wanafanyishwa mazoezi makali ndani ya mahema yenye joto na kuvaa fulana za barafu kabla ya mechi na wakati wa mapumziko.

Kansas City ambako England wataweka kambi kuanzia Juni 13 pia inatarajiwa kuwa na joto la zaidi ya 32°C, ambalo kwa Wazungu huwasumbua.

Wanasoka wanaweza kutokwa na jasho hadi lita tano (pinti 8.9) wakati wa mechi, wakipoteza karibu kilo moja ya uzito katika viwanja vyenye joto kali, utafiti unaonyesha.

Andrew Simms, mkurugenzi wa New Weather Institute, anasema: “Usalama wa wachezaji ni suala la haraka na la dharura, mambo yanaweza kwenda vibaya haraka sana watu wakipata joto kupita kiasi. Tuna wasiwasi kwamba Fifa inacheza kamari isiyo ya busara na afya na usalama wa wachezaji.”

Ndege zisizo na rubani (drones) zitapigwa marufuku kuruka juu ya viwanja vya Marekani vitakavyotumika kwenye mechi za Kombe la Dunia pamoja na maeneo ya mashabiki, mamlaka zimeshasema, lakini gumzo linaweza kuwa ni jinsi wake na wapenzi wa wanasoka hasa wa England watanavyoitikisa miji ambako timu hiyo itatua kucheza mechi au nyakati za mazoezi.