Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Mudryk kwenye msala huu

Muktasari:


  • Staa huyu ambaye hajaonekana katika mechi tano zilizopita amesimamishwa kwa muda kwa ajili ya kuwasilisha utetezi wake kabla ya hukumu kamili kutoka juu ya miezi mingapi atafungiwa.

LONDON, ENGLAND: WIKI hii staa wa Chelsea Mykhailo Mudryk amesimamishwa kucheza soka baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa zilizokatazwa michezoni.

Staa huyu ambaye hajaonekana katika mechi tano zilizopita amesimamishwa kwa muda kwa ajili ya kuwasilisha utetezi wake kabla ya hukumu kamili kutoka juu ya miezi mingapi atafungiwa.

Kwa mwaka huu amekuwa mchezaji mwingine maarufu kukutwa na matumizi ya dawa hizo za kuongeza nguvu zilizopigwa marufu michezo.

Hata hivyo, kuna kundi kubwa la wachezaji ambao wamewahi kukutana na vifungo virefu kwa matumizi ya dawa hizi.

Hawa hapa ni wachezaji watano waliokutwa na hatia na kukumbana na vifungo virefu.


MARK BOSNICH - Miezi 8

Hadithi ya adhabu ya Mark Bosnich ni moja ya mambo ambayo yanasikitisha. Katika kikao cha nidhamu, mchezaji huyu wa kimataifa wa Australia alikutwa na hatia ya mashtaka mawili yaliyotolewa dhidi yake, kwanza kwa utofu wa nidhamu na pili kwa kupatikana na matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.

Hata hivyo, licha ya kuhukumiwa, Bosnich alikataa kuhusika na suala hili na kusisitiza dawa hizo alitumia bila ya kujua.

Alifungiwa miezi tisa kujihusisha na michezo na jambo baya ni kwamba baada ya hapo aliangukia katika uraibu wa matumizi ya dawa za kulevya.


ANDRE ONANA - Miezi 9

Huyu alitumia dawa aina ya PEDs  ambazo zinatajwa kuongeza ufanisi na utendaji. Tukio hili lilijiri  baada ya sare ya 2-2 na Atalanta.

Onana, ambaye alikuwa akichezea Ajax wakati huo, alidai alikumbwa na maumivu makali ya kichwa, akatumia paracetamol ili kupunguza maumivu.

Baada ya hapo, alipimwa na klabu yake  na siku mbili baadaye matokeo yakatoka ametumia dawa ambazo haziruhusiwi michezoni.

Baada ya hapo alifungiwa miezi tisa.


DIEGO MARADONA- Miezi 15

Amewahi kukutana na adhabu mara mbili juu ya matumizi ya dawa hizi zisizoruhusiwa michezoni.

Diego Maradona alifungiwa kucheza soka mara mbili, zote kwa miaka  miezi 15. Ya kwanza ilitokea mwaka 1991, alipogundulika ametumia kokeini wakati akiwa na Napoli na kufungiwa kucheza kwa miezi 15.

Licha ya adhabu hii, Maradona alirejea na kuonyesha kiwango bora kiasi cha kujumuishwa tena katika kikosi cha Argentina cha Kombe la Dunia la 1994.

Akiwa katika michuano hiyo pia alikutwa na matumizi ya dawa zilizokatazwa na kufungiwa tena miezi 15.


ROMAN EREMENKO – Miezi 24

 Roman Eremenko ambaye sio mchezaji anayejulikana sana, alikumbana na moja kati ya adhabu za muda mrefu baada ya kukutwa na hatia ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu. 

Mnamo Oktoba 6, 2016, mchezaji huyu wa kimataifa wa Finland alipewa adhabu ya kusimamishwa kwa siku 30 na UEFA, kwa ajili ya kupisha uchunguzi na baada ya hapo alifungiwa kwa miaka miwili mnamo Novemba 18, 2016. Kiungo huyo wa zamani wa CSKA Moscow alikutwa na matumizi ya kokeini na licha ya kukata rufaa bado adhabu ilimkumba. Eremenko alihudumu kwa muda mrefu katika timu mbalimbali huko Urusi na hata baada ya kuruhusiwa kucheza alizitumikia  Spartak Moscow na Rostov.  Akiwa na umri wa miaka 37, kwa sasa anaichezea IF Gnistan.


PAUL POGBA - Miezi 48

Ni miongoni mwa stori zilizotikisa sana kwa mwaka huu. Awali staa huyu wa kimataifa wa Ufaramsa alifungiwa miaka minne Februari mwaka huu baada ya kufanyiwa vipimo Septemba mwaka jana na mamlaka za udhibiti wa matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezo ya Italia, NADO, baada ya mchezo wa ligi, kati ya timu yake  Juventus dhidi ya Udinese, Agosti, 2023.

Awali staa huyu alifungiwa miaka minne lakini alikata rufaa kwenda CAS na adhabu yake ikapunguzwa kufikia miezi 18 na atarejea tena uwanjani Machi mwakani.