Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili tano za kusubiri hizi hapa

DILI Pict

Muktasari:

  • Baada ya kuondoka kwa mastaa matata kabisa kama Kevin De Bruyne walijiojengea umaarufu mkubwa kwenye ligi hiyo, mashabiki sasa wanasubiri kuona ni wakali gani wengine watakaoingia kwenye dirisha hili ili kuja kuleta utamu zaidi kwa msimu ujao.

LONDON, ENGLAND: DIRISHA la usajili wa wachezaji la majira ya kiangazi limeshafunguliwa tangu Juni Mosi na sasa klabu zipo bize kwelikweli kusaka wachezaji mwafaka wa kuboresha vikosi vyao kwa ajili ya msimu wa 2025/26.

Baada ya kuondoka kwa mastaa matata kabisa kama Kevin De Bruyne walijiojengea umaarufu mkubwa kwenye ligi hiyo, mashabiki sasa wanasubiri kuona ni wakali gani wengine watakaoingia kwenye dirisha hili ili kuja kuleta utamu zaidi kwa msimu ujao.

Kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kwa upande wa Ligi Kuu England, vipaumbele vikuu kwa timu ni kwenye kusajili Namba 9 na Namba 10 wa viwango vya dunia.

Kutokana na hilo, hii hapa orodha ya mastaa watano matata kabisa wanaotarajiwa kunaswa na timu za Ligi Kuu England katika dirisha hili ili kuja kukipiga kwenye ligi hiyo msimu ujao.

DIL 01

1. Viktor Gyokeres

Anatajwa kama straika matata kabisa Ulaya kwa sasa kutokana na kile anachofanya huko Sporting Lisbon baada ya kuwa na wakati mgumu Brighton na Swansea City wakati akiwa kinda.

Gyokeres aliibuka na kuwa balaa uwanjani kipindi yupo chini ya kocha Ruben Amorim huko Sporting, ambaye alijipambanua na kuwa straika wa mabao.

Kwa msimu uliopita, Gyokeres alifunga mabao 39 katika mechi 33 kwenye Primeira Liga na mabao sita alifunga kwenye mechi nane za Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa misimu yake miwili huko Ureno, Gyokeres amefunga mabao 79 katika mechi 83 alizocheza Primeira Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Manchester United na Arsenal zinafukuzia huduma yake na kuna uwezekano akanaswa katika dirisha hili.

DIL 02

2. Benjamin Sesko

Hana makali ya kufunga sana kama ambavyo Gyokeres amekuwa akifanya, lakini Sesko ni moja ya mastraika mahiri kwenye soka la Ulaya kwa sasa.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 22, amefunga mabao 21 katika mechi 45 za michuano yote aliyochezea RB Leipzig msimu uliopita, yakiwamo mabao 13 aliyofunga kwenye Bundesliga na manne aliyofunga katika mechi sita za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mabao yake mawili aliyofunga dhidi ya Juventus kwenye michuano ya Ulaya yalionyesha jinsi Sesko alivyopevuka na kuwa kivutio kikubwa kwa klabu kubwa zinazotaka saini yake. Chelsea na Arsenal zinamhitaji kwa nguvu.

DIL 03

3. Hugo Ekitike

Ekitike ni dili safi. Straika huyo mwenye umri wa miaka 22 amefunga mabao 15 na kuasisti manane katika mechi 33 alizocheza katika Bundesliga akikitumikia kikosi cha Eintracht Frankfurt msimu uliopita.

Si Namba 9 wengi wenye uwezo wa kuwa wabunifu ndani ya uwanja kama ambavyo Ekitike amekuwa akifanya.

Staa huyo ametengeneza nafasi za mashambulizi 44, akiwa ni miongoni mwa waliofanya hivyo mara nyingi kwenye ligi kwa wachezaji wanaocheza katika eneo la washambuliaji wa kati, huku akijaribu kupita na mpira mbele ya mabeki wa timu pinzani mara 126.

Ekitike ni straika, lakini staili yake ya uchezaji inampa nafasi ya kutumika kama Namba 10 wa kisasa kabisa. Yupo kwenye rada za Chelsea wakimhitaji Stamford Bridge.

DIL 04

4. Rayan Cherki

Mchezaji mwingine aliyeonyesha kiwango bora kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita ni mkali Cherki mwenye umri wa miaka 22.

Zao hilo la kutokea kwenye akademia ya Lyon amekuwa mchezaji muhimu sana kwa timu yake katika msimu wa 2024/25.

Alichangia mabao 19 kwa maana ya kufunga au kuasisti katika mechi 22 alizoanzishwa kwenye Ligue 1, huku mabao mengine 12 alifunga katika mechi 11 alizoanzishwa katika Europa League, takwimu ambazo zimevutia timu nyingi za Ligi Kuu England kuhitaji saini yake.

Staili yake ya kukokota mpira imemfanya Cherki alinganishwe na Lionel Messi huku Manchester City ikitajwa kutaka saini yake na msimu ujao huenda akaonekana akiwa na uzi wa wakali hao wa Etihad.

DIL 05

5. Florian Wirtz

Kiungo mshambuliaji Wirtz ni miongoni mwa wachezaji wanaosubiriwa kwa hamu watue kwenye Ligi Kuu England wakati wa dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya mkali huyo wa Bayer Leverkusen kuwekwa kwenye rada za Liverpool.

Kocha Arne Slot, anahitaji saini ya mkali huyo mwenye umri wa miaka 22, akitaka akafanye majukumu ya kutawala katika Namba 10 kushindana na wafundi wengine matata kabisa kwenye eneo hilo.

Kwa misimu miwili iliyopita, Wirtz amehusika kwenye mabao 67 katika mechi 75 katika michuano yote aliyochezea Bayer Leverkusen, akiwa amefunga mara 34 na asisti 33.