Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Saudi Arabia laivuruga Aston Villa

ASTON Pict

Muktasari:

  • Villa imesema tayari imekataa ofa nne kutoka kwa Al-Hilal, inayoshiriki Ligi Kuu Saudi Arabia, kwa ajili ya Watkins. Ofa ya mwisho inadaiwa kuwa na thamani ya karibu Pauni 34 milioni (zaidi ya Sh95 bilioni), lakini hiyo ni bei ambayo Villa haitaki kumuuza mchezaji huyo kwa kiasi hicho.

BRIGHTON, ENGLAND: KOCHA wa Aston Villa, Unai Emery, amedokeza kwa nguvu kwamba mshambuliaji wake Ollie Watkins huenda alikuwa hataki kuichezea timu hiyo, wakati Villa ikipokea kichapo kizito cha mabao 4-0 kutoka kwa Brighton, huku kukiwa na tetesi za ofa kutoka kwa klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia kwa ajili ya straika huyo.

Villa imesema tayari imekataa ofa nne kutoka kwa Al-Hilal, inayoshiriki Ligi Kuu Saudi Arabia, kwa ajili ya Watkins. Ofa ya mwisho inadaiwa kuwa na thamani ya karibu Pauni 34 milioni (zaidi ya Sh95 bilioni), lakini hiyo ni bei ambayo Villa haitaki kumuuza mchezaji huyo kwa kiasi hicho.

Mshambuliaji huyo wa England hakujumuishwa kwenye kikosi cha Villa kilichopoteza 4-0, licha ya kwamba washambuliaji wengine wawili pekee waliopo kikosini, Brian Madjo na Tammy Abraham wote wakiwa majeruhi.

Kwa mujibu wa taarifa zinazohusu upande wa Villa, inaeleweka kuwa Watkins si mgonjwa wala hajajeruhiwa. Hata hivyo, inaami nika hakufanya mazoezi yote kikamilifu wiki iliyopita. Mwakilishi wa Watkins ameshaombwa kutoa maoni yake kuhusu suala hilo.

Akizungumzia msimamo wa Watkins, Emery alisema: “Swali hili ni kwa ajili yake. Mimi naweza kujibu kwa ukimya wangu tu.”

Alipoulizwa kama Watkins alikataa kucheza, Emery akajibu: “Nadhani unaweza kumpigia simu, unaweza kumpigia simu wakala wake na yeye anaweza kujibu.”

ASTO 04

Emery pia aliulizwa kama alihisi amesalitiwa au kuvunjwa moyo na Watkins, ambaye amekuwa akionyesha maendeleo makubwa chini ya kocha huyo.

Akajibu: “Ni yeye pekee anayeweza kueleza jibu lake, siwezi mimi. Tulikuwa na washambuliaji wawili waliojeruhiwa na mshambuliaji mwingine ni jibu lake.”

Katika moja ya mechi mbaya zaidi za Villa tangu Emery alipoanza kuinoa, timu hiyo yenye sura mpya ilipasuliwa vibaya na Brighton, huku kiungo Joao Gomes akitolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu akiwa na Villa.

Brighton ilifika mabao manne ndani ya dakika 31 tu, huku Villa ikionekana kutokuwa na majibu dhidi ya mashambulizi ya wenyeji.

Kwa kiasi kikubwa kutokana na kanuni za kifedha za UEFA, Villa imeuza wachezaji wenye thamani ya takribani pauni 250 milioni katika dirisha hili la usajili.

ASTO 03

Morgan Rogers, Youri Tielemans, Lucas Digne na Ezri Konsa wote wameondoka, huku Watkins na kipa Emi Martinez ambaye pia hakuwapo katika mchezo huo wakitajwa wanaweza kufuata mkondo huo.

Wachezaji hao wote sita walikuwa nguzo muhimu ya kikosi cha Villa kilichoichapa Freiburg kwa mabao 3-0 mwezi Mei na kutwaa taji la Europa League.

Villa imekuwa ikipata changamoto mara kwa mara wakati dirisha la usajili linapokuwa wazi, jambo lililomfanya Emery kutoa utani baada ya mchezo huo akisema: “Nadhani dirisha la usajili linapaswa kuwa limefungwa muda wote.”

Emery aliongeza: “Katika miaka mitatu iliyopita, hadi dirisha la usajili linapofungwa, tumekuwa na matatizo kama haya tunayopitia sasa. Wachezaji wana mentaliti ninayoitaka hawalalamiki, hawalaumu, na wanajaribu kuwa na subira, hata kwa matokeo kama ya leo.

ASTO 01

“Tumekuwa na tatizo hili (la dirisha la usajili) kila msimu na tumeliweza kulishinda. Lakini ni jambo gumu kwetu kila mwaka.”

Kwa upande mwingine, Brighton nayo imewapoteza baadhi ya wachezaji wake muhimu na kuna wasiwasi kuhusu hatima ya Yankuba Minteh na Carlos Baleba.

Kocha Fabian Hurzeler alisema Minteh ana tatizo la kifundo cha mguu, wakati Baleba anahusishwa kuondoka klabuni hapo kujiunga na Man United.

Minteh anawindwa na Liverpool, huku Manchester United ikimtaka Baleba. Wachezaji hao wawili hawakushiriki katika mchezo huo dhidi ya Villa.

Brighton ilifunga mabao manne ndani ya dakika 31, ikianza kwa bao la kujifunga la Victor Lindelof, kabla Maxim De Cuyper kufunga bao la pili kwa kugusa mpira uliokuwa ukielekea langoni.

Jack Hinshelwood kisha akafunga mabao mawili kwa haraka na kuiwezesha Brighton kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa tofauti kubwa.

Hurzeler alisema kadi nyekundu ilikuwa sababu nyingine iliyobadilisha kabisa mwelekeo wa mchezo, lakini alifurahishwa na namna timu yake ilivyocheza kipindi cha pili.

“Kadi nyekundu ilikuwa sababu nyingine iliyobadilisha mchezo na tulicheza kipindi cha pili kwa ukomavu, kwa sababu si rahisi kupata uwiano mzuri unapokuwa na mchezaji mmoja zaidi,” alisema Hurzeler.

“Nilifurahia sana kiwango cha uchezaji wetu.”