Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Gyokeres, vigogo Arsenal watua Ureno

Muktasari:

  • Hadi sasa bado vigogo hao wapo nchini Ureno kwa ajili ya mazungumzo kwani bado hawajafikia mwafaka juu ya dili hilo kwa upande wa mchezaji.

ARSENAL imefanya mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa Sporting, Viktor Gyokeres, jijini Lisbon na imetoa ofa ya Pauni 59 milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden.

Hadi sasa bado vigogo hao wapo nchini Ureno kwa ajili ya mazungumzo kwani bado hawajafikia mwafaka juu ya dili hilo kwa upande wa mchezaji.

Mkataba wa Gyokeres unatarajiwa kumalizika Juni 30, 2028 na Sporting imeripotiwa kuwa tayari kumwachia kwa kiasi cha Pauni 59 milioni kwa sababu ya heshima aliyoonyesha baada ya kukataa kuondoka katika dirisha lililopita la majira ya baridi licha ya kupokea ofa nono.

Katika msimu uliomalizika, fundi huyu alicheza mechi 52 za michuano yote, akafunga mabao 54 na kutoa asisti 13.


LIAM DELAP

MANCHESTER United imeshafikia makubaliana ya kumsajili straika wa Ipswich Town, Liam Delap na mabosi wa timu hiyo sasa wanasubiri kauli ya Delap mwenyewe ikiwa atakuwa tayari kujiunga nayo katika dirisha lijalo au laa.

Delap ambaye ni miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango bora kwa msimu uliopita, mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2029.


CRISTIANO RONALDO

MSHAMBULIAJI wa Ureno, Cristiano Ronaldo, mwenye umri wa miaka 40, anatarajiwa kuondoka katika klabu ya Al-Nassr ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia na kujiunga na timu mpya ili kushiriki Kombe la Dunia la Klabu linaloanza Juni 15, nchini Marekani.

Ronaldo ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu huu, kiujumla akiwa na Al Nassr, amehusika katika mabao 118 katika mechi 111, akifunga mabao 99 na kutoa asisti 19.


Rayan Cherki

MANCHESTER City inamhitaji kiungo wa  Olympique Lyon, Rayan Cherki, mwenye umri wa miaka 21, ambaye pia amehusishwa na Liverpool na Chelsea kuelekea dirisha lijalo.

Cherki ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, amecheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao 12. Amesifika kwa uwezo wake wa kuficha mali mguuni.


Callum Wilson

EVERTON imejumuika pamoja na Leeds United katika vita ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Newcastle na timu ya taifa ya England, Callum Wilson, mwenye umri wa miaka 33, ambaye mkataba wake unaisha mwezi ujao.

Callum ni miongoni mwa mastaa ambao wameomba kuondoka Newcastle kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine. Amekuwa hana namba ya kudumu kikosini.


Leroy Sane

TOTTENHAM imepewa nafasi ya kumsajili winga wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Leroy Sane, mwenye umri wa miaka 29, ambaye atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa mwezi ujao.

Inaelezwa wawakilishi wa Sane kwa sasa wapo nchini England ambako wametua kwa ajili ya kufanya mazungumzo na wawakilishi wa timu mbalimbali.


Cody Gakpo

KOCHA wa Liverpool, Arne Slot, anataka kumbakisha mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi, Cody Gakpo, 26, licha ya Bayern Munich kuonyesha nia ya kutaka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Gakpo ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu huu amecheza mechi 49 za michuano yote na kufunga mabao 18.


Nahuel Molina

NEWCASTLE ina matumaini ya kuzipiku Napoli, Juventus na Roma kwenye vita ya kuiwania saini ya beki wa kulia wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Argentina, Nahuel Molina, 27. Molina ambaye ameonyesha kiwango bora kwa msimu huu, mkataba wake unaisha 2027, msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote.