Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Darwin Nunez awekwa sokoni rasmi Liverpool

Nunez Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa Slot hafurahishwi na kiwango cha fundi huyu raia wa Uruguay na anahitaji auzwe ili asajiliwe mshambuliaji mwingine ambaye ataendana na vile anavyotaka.

STRAIKA wa Liverpool, Darwin Nunez inadaiwa ni mmoja wa wachezaji walipewa ruhusa ya kuondoka timu hiyo dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa Slot hafurahishwi na kiwango cha fundi huyu raia wa Uruguay na anahitaji auzwe ili asajiliwe mshambuliaji mwingine ambaye ataendana na vile anavyotaka.

Timu mbalimbali zinatajwa kutaka kumsajili Nunez ikiwa pamoja na Al Nassr iliyoonyesha nia hiyo dirisha lililopita la majira ya baridi.

Tangu kuanza kwa msimu huu, staa huyu aliyejiunga na Liverpool akitokea Benfica mwaka 2028, amecheza mechi 35 za michuano yote, akafunga mabao sita na kutoa asisti tano.

Hata hivyo mashabiki wamekuwa wakimlalamikia juu ya nafasi nyingi za wazi anazozikosa mara kwa mara.


Frenkie de Jong

INAELEZWA Liverpool inataka kufanya kazi ya ziada katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kuboresha kikosi na moja kati ya majina ambayo benchi la ufundi limeyaweka katika mpango kazi ni la kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi, Frenkie de Jong, 27, ambaye hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha timu yake. Mkataba wa De Jong unatarajiwa kumalizika 2027 na nyota huyo amekuwa akitakiwa pia na miamba ya England Manchester United kwa muda mrefu.


Rafael Leao

AC Milan ipo tayari kusikiliza ofa kutoka kwa timu zinazohitaji saini ya winga wao raia wa Ureno,  Rafael Leao, 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Huduma ya winga huyu anayeweza kuuzwa kwa zaidi ya Pauni 60 milioni, inahitajika na Barcelona na Chelsea ambazo zilijaribu kutaka kumsajili tangu Januari mwaka huu. Leao amekuwa hapati namba katika kikosi cha kwanza cha AC Milan na kuna uwezekano akasepa.


Juan Musso

Manchester United inataka kumsajili kipa wa Atalanta na timu ya taifa ya Argentina, Juan Musso, 30, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Atletico Madrid. Benchi la ufundi la Man United linataka kumsajili Musso kama sehemu ya kumpa changamoto kipa wao namba moja raia wa Cameroon Andre Onana. Akiwa na Atletico Musso amecheza mechi nane za michuano yote na amekuwa katika kiwango kizuri.


Bryan Mbeumo

NEWCASTLE United inataka kulipa Pauni 50 milioni ili kuipata saini ya mshambuliaji wa Brentford na timu ya taifa ya Cameroon, Bryan Mbeumo ambaye ameonyesha kiwango bora akiwa na Brentford tangu kuanza kwa msimu huu. Mbeumo mwenye umri wa miaka 25, kiwango chake kimesababisha timu nyingi kubwa kuhitaji saini yake na mbali ya Newcastle United, Arsenal na Liverpool pia zimekuwa zikitajwa kuwania saini yake.


Theo Hernandez

BEKI wa AC Milan raia wa Ufaransa, Theo Hernandez, 27, yupo kwenye rada za Manchester United inayohitaji kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Man United inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili beki huyu wa kushoto kwa sababu Milan imeshaonyesha utayari wa kumuuza ikiwa mchezaji mwenyewe atahitaji hilo litokee.


Martin Dubravka

NEWCASTLE United imefikia makubaliano ya kumuongeza mkataba mpya kipa wao raia wa Slovakia, Martin Dubravka, 36, kabla ya dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu. Kipa huyu ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwakani, awali alikuwa akiwindwa na timu za Saudi Arabia lakini alikataa kujiunga nazo na kusalia Newcastle.


Mason Greenwood

Barcelona, Bayern Munich na PSG zipo vitani kuiwania saini ya mshambuliaji wa Marseille,  Mason Greenwood, 23, dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwenye dili ambalo Man Uniter itafaidika kwa kupata asilimia 50 ya mauzo yake. Greenwood amevutia vigogo hawa kutokana na kiwango bora alichoonyesha akiwa na Marseille.