Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WATAWEZA? Rekodi ya Ronaldo inayowasubiri Mbappe, Haaland Ligi ya Mabingwa

WATAWEZA Pict

Muktasari:

  • Jose Mourinho alirejea kwenye michuano hiyo akiiongoza Real Madrid kupata ushindi licha ya kutawala mpira kwa muda mfupi. Wakati huo huo, Manchester City ilipata ushindi wa kirahisi dhidi ya Porto. Lakini, katikati ya matukio yote yaliyotarajiwa katika michezo yote iliyochezwa yalikuwa mabao yaliyofungwa na Mbappe na Haaland.

MADRID, HIPANIA: KYLIAN Mbappe na Erling Haaland walianza kampeni ya 2026-27 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufunga mabao Jumanne, wiki hii, ambapo wote wawili watakuwa wakiiangalia rekodi ya muda wote ya mabao katika mashindano hayo.

Jose Mourinho alirejea kwenye michuano hiyo akiiongoza Real Madrid kupata ushindi licha ya kutawala mpira kwa muda mfupi. Wakati huo huo, Manchester City ilipata ushindi wa kirahisi dhidi ya Porto. Lakini, katikati ya matukio yote yaliyotarajiwa katika michezo yote iliyochezwa yalikuwa mabao yaliyofungwa na Mbappe na Haaland.

Mbappe alifungua ukurasa wa mabao kwa kumalizia kwa ustadi baada ya kutumia kosa la Yann Bisseck, na kuipa Madrid mwanzo wa ushindi wa 2-1 dhidi ya Inter Milan wakati Haaland alifunga mabao mawili na kuipa Man City ushindi wa 2-0 nchini Ureno.

Mbali na kusaidia kuhakikisha timu zao zinaanza kwa ushindi kampeni ya hatua ya ligi ya 2026-27, mabao hayo pia yaliwasaidia wachezaji hao kupanda zaidi katika orodha ya wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa. Tangu mashindano hayo yalipopewa jina jipya mwaka 1992, wote wawili wameingia katika orodha ya wachezaji saba bora kwa idadi ya mabao.

Mbappe bado ana umri wa miaka 27, wakati Haaland ni mdogo zaidi akiwa na 26, hivyo wote wanaweza kucheza katika mashindano hayo kwa miaka 10 ijayo. Huenda wasiendelee kufunga mabao katika ligi hiyo kwa kasi ya ajabu waliyonayo sasa kwa muongo mwingine, lakini wote wanaweza kuwa wakiiangalia rekodi ya Ronaldo ya mabao 140.

ZAM 02

Mbappe kwa sasa anashika nafasi ya tano kwa pamoja katika orodha hiyo. Bao lake la Jumanne lilimfanya afikie mabao 51 ya Ligi ya Mabingwa sawa na gwiji wa Madrid, Raul Gonzalez, ingawa Mbappe alifikisha idadi hiyo katika mechi 99, ikilinganishwa na mechi 142 za Mhispania huyo. Mbappe anafunga bao katika mashindano hayo kila baada ya dakika 112.4 kwa wastani, kiwango ambacho ni cha sita kwa ubora miongoni mwa wachezaji 27 waliofunga angalau mabao 30 katika mashindano hayo.

Haaland yupo chini zaidi katika orodha ya wafungaji, lakini ana faida ya umri na anafunga kwa kasi ambayo haijawahi kufikiwa na mchezaji mwingine katika historia ya mashindano hayo.

Yupo nafasi ya saba akiwa na mabao 59 katika mechi 59 pekee, akifunga bao kila baada ya dakika 79.7, jambo ambalo kwa kutarajiwa ni kiwango bora zaidi kwa mbali miongoni mwa kundi hilo la wachezaji. Lionel Messi ndiye anayemkaribia Haaland kwa takwimu hiyo, akiwa alifunga bao kila baada ya dakika 105.3 katika katika kipindi cha maisha yake ya soka.

Kwa hiyo, mashine hizi mbili za mabao zina nafasi gani ya kumfikia Ronaldo? Mshambuliaji huyo Mreno alifunga mabao 140 katika mechi 183, akiwa na wastani wa bao moja kila baada ya dakika 113.9. Kiwango hicho kinafanana karibu kabisa na cha Mbappe, jambo linaloashiria kuwa Mfaransa huyo atalazimika kucheza idadi ya mechi inayokaribia ya Ronaldo katika mashindano hayo ikiwa anataka kuvunja rekodi hiyo.

Tayari amecheza mechi 99, maana yake anahitaji kucheza mechi nyingine 84 ili kufikia 183 za Ronaldo, ambazo pia ni rekodi ya mashindano hayo. Hata hivyo, Mbappe ana faida kutokana na Ligi ya Mabingwa kupanuliwa, ambapo sasa timu yoyote inayofika hatua ya ligi itacheza angalau mechi nane na timu zinazofika fainali zinaweza kucheza hadi mechi 17.

Kwa hiyo, inawezekana, ingawa ni jambo lisilowezekana sana kwa Mbappe kucheza mechi hizo 84 za lii hiyo katika misimu mitano ijayo. Ikiwa ataendelea kufunga kwa kiwango cha sasa, anaweza kuvunja rekodi ya Ronaldo katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ya msimu wa 2030-31.

WAKA 01

Hilo litahitaji Real Madrid au klabu yoyote ambayo Mbappe atakuwa akiichezea kufika fainali na pia kucheza hatua ya mchujo katika kila mmoja wa misimu mitano ijayo. Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa ikamchukua misimu mingine miwili kufikisha idadi ya mechi anazohitaji.

Hilo linaweza kumaanisha Mbappe kuvunja rekodi ya mabao ya michuano hiyo ndani ya miaka saba wakati huo akiwa na miaka 34. Ukizingatia kupungua kwa kasi ya ufungaji mabao katika miaka yake ya katikati ya 30, anaweza kuwa na miaka michache ya ziada ya kumfuatilia Ronaldo.

Haaland anaweza kuwa nyuma ya Mbappe kwa mabao 12 wakati wa kuandikwa kwa makala hii, lakini kiwango chake cha kipekee cha kufunga kinamfanya kuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuwania nafasi ya kwanza katika orodha hii.

Na licha ya kuwa ana faida ya umri, kama ilivyoonyeshwa hapo juu ni kiwango chake cha kufunga bao moja kwa kila mchezo kinachomuweka katika nafasi nzuri ya kuvunja rekodi hiyo, kama inavyoonyeshwa hapa chini. Atahitaji kucheza mechi nyingine 82 ili kumpita Ronaldo, jambo ambalo, kama ilivyo kwa Mbappe, linaweza kutokea ndani ya misimu mitano ijayo.

ZAM 03

Hata hivyo, kwa kuzingatia kwamba Man City haijawahi kufika zaidi ya robo fainali tangu ilipotwaa ubingwa wa mashindano hayo msimu wa 2022-23, na hata ilitolewa katika hatua ya mchujo msimu wa 2024-25, hakuna uhakika kwamba itaweza kufika mbali katika mashindano hayo kwa misimu mitano mfululizo.

Ikiwa klabu ambayo Haaland atakuwa akiichezea itacheza wastani wa mechi 12 za Ligi ya Mabingwa kwa msimu, jambo ambalo lingemaanisha kufika robo fainali bila kucheza hatua ya mchujo au kufika hatua ya 16 bora kupitia hatua ya mchujo, atahitaji misimu 6.83 ya kuendelea kufunga kwa kiwango chake cha sasa.

Hilo litamaanisha kuwa akiwa asilimia 83 ya msimu wa 2033-34 ambao utakuwa mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora, Haaland angefunga bao litakalomfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ligi ya Mabingwa.

Na kwa kuwa ni mdogo kuliko Mbappe anaweza pia kuendelea kufunga kwa muda mrefu zaidi ya mpinzani wake katika mbio hizi za rekodi. Kwa hiyo, ikiwa mastaa hao wawili wataendelea kufunga kwa kiwango walichoanza nacho, zitashuhudiwa mbio za kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ligi ya Mabingwa Ulay zikifikia kilele katikati ya miaka ya 2030. Hilo ni jambo la kusubiri na kuona.