Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cristiano Ronaldo anukia Brazil

Muktasari:

  • Timu za Brazil ambazo zimefuzu kucheza michuano hiyo itakayopigwa Marekani kuanzia mwezi ujao ni pamoja na Palmeiras, Flamengo, Fluminense na Botafogo, hivyo moja kati ya hizi anaweza kujiunga nazo.

MSHAMBULIAJI wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo, mwenye umri wa miaka 40, amepokea ofa kutoka kwa timu moja ya Brazil, ambayo itamruhusu nyota huyo wa kimataifa wa Ureno kucheza mashindano ya Kombe la Dunia la Klabu ikiwa atajiunga nayo.

Timu za Brazil ambazo zimefuzu kucheza michuano hiyo itakayopigwa Marekani kuanzia mwezi ujao ni pamoja na Palmeiras, Flamengo, Fluminense na Botafogo, hivyo moja kati ya hizi anaweza kujiunga nazo.

Ripoti zinaeleza Ronaldo ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, hataongeza mkataba akidaiwa kutaka kupata changamoto mpya sehemu nyingine.

Vilevile staa huyu anataka kuondoka baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa barani Asia kwa msimu ujao na hana maelewano mazuri na baadhi ya viongozi wa Al-Nassr ambao wamechukizwa na vitendo vyake vya kuondoka uwanjani bila ya kwenda vyumba vya kubadilishia nguo kwa wachezaji wenzake mara baada ya mechi kumalizika.

Tangu ametua katika Ligi Kuu ya Saudi Arabia, Ronaldo ameipa umaarufu mkubwa michuano hiyo kufuatiliwa dunia nzima, huku pia akichangia mastaa wengi duniani kukubali ofa za kujiunga na timu za Saudia, licha ya kwamba ligi hiyo haikuwa ikichukuliwa kama ni ya ushindani.


Bryan Mbeumo

MANCHESTER United imetoa ofa ya Euro 65 milioni kwenda Brentford kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Cameroon, Bryan Mbeumo, mwenye umri wa miaka 25, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa.

Mbeumo amekuwa akiwindwa na timu nyingi kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu.


Ferran Torres

ASTON Villa wanavutiwa na mshambuliaji wa Barcelona, Ferran Torres, mwenye umri wa miaka 25, na wako tayari kutoa takriban Euro 50 milioni kwa ajili ya kuipata saini yake katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Torres amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Barca kwa msimu huu na ameonyesha nia ya kutaka kuondoka kujiunga na timu itakayompa nafasi kubwa zaidi ya kucheza.


Rayan Cherki

WINGA wa Olympique Lyon na timu ya taifa ya  Ufaransa, Rayan Cherki, mwenye umri wa miaka 21, ambaye ameweka wazi kwamba ataondoka mwisho wa msimu huu, yupo kwenye rada za vigogo mbalimbali barani Ulaya ikiwa pamoja na Manchester United na Liverpool.

Tangu kuanza kwa msimu huu Cherki amecheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao 12.

Pedro Goncalves

MANCHESTER United wanavutiwa na kiungo wa Sporting na Ureno, Pedro Goncalves, 26, ambaye wanatarajia kuanza mazungumzo na wawakilishi wake hivi karibuni.

Pedro ambaye msimu huu amechukua ubingwa akiwa na Lisbon, amekuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha wababe hao kwa muda mrefu.


Leroy Sane

MABOSI wa Bayern Munich bado hawajakata tamaa ya kumbakisha winga wao Leroy Sane, katika kikosi kwa msimu ujao licha ya mkataba wake kuwa unamalizika mwisho wa msimu huu.

Sane mwenye umri wa miaka 29, anadaiwa kuwa amekataa ofa ya Bayern ya mkataba mpya aliyopewa hivi karibuni akihitaji kiasi kikubwa zaidi ya kile ambacho timu hiyo iko tayari kumpa.


Morgan Gibbs-White

NOTTINGHAM Forest inapambana kuwapa mikataba mipya haraka iwezekanavyo wachezaji wao wa kimataifa wa England, kiungo Morgan Gibbs-White, 25, na winga Callum Hudson-Odoi, 24, ambao wameonyesha kiwango bora kwa msimu uliopita. Mabosi wa Nottingham wana wasiwasi kuwa vigogo wanaweza kupiga hodi ili kuhitaji huduma zao.


Jonathan David

NAPOLI inahitaji mshambuliaji wa kati na inapanga kumsajili staa wa Lille na timu ya taifa ya Canada, Jonathan David, 25, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo, ikiwa itashindwa kumpata inaweza kuhamia kwa mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay, Darwin Nunez, mwenye umri wa miaka 25.