Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chiesa aingia anga za Napoli kumrithi Khvicha

Muktasari:

  • Chiesa hapati nafasi ya kutosha Liverpool kwa sasa na kumekuwa na tetesi zinazoeleza anaweza akatolewa kwa mkopo ama kuuzwa Januari ingawa kocha wa majogoo hao, Arne Slot amefunguka bado yupo katika mipango yake.

NAPOLI imepanga kumsajili winga wa Liverpool, Federico Chiesa, 27, dirisha lijalo ili akazibe pengo la mshambuliaji wao raia wa Georgia, Khvicha Kvaratskhelia ambaye anahusishwa kuondoka Januari mwakani na anawindwa na Chelsea, Barcelona na Manchester United.

Chiesa hapati nafasi ya kutosha Liverpool kwa sasa na kumekuwa na tetesi zinazoeleza anaweza akatolewa kwa mkopo ama kuuzwa Januari ingawa kocha wa majogoo hao, Arne Slot amefunguka bado yupo katika mipango yake.

Kwa sasa staa huyu wa kimataifa wa Italia anauguza majeraha na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi tatu za michuano yote na kutoa asisti moja.

Mkataba wa sasa wa Chiesa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, wakati ule wa Khvicha ukimalizika mwaka 2027.


JUVENTUS imetuma maombi ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Joshua Zirkzee kwa mkopo wa nusu msimu katika dirisha la majira ya baridi Januari mwakani. Staa huyu wa kimataifa wa Uholanzi, amejiunga na Man United dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini hajaonyesha kiwango kilichotarajiwa na mashabiki wengi wa mashetani hao wekundu na huenda asiwe kwenye mipango ya kocha mpya Ruben Amorim msimu ujao.


PARIS St-Germain inataka kumtoa staa wao raia wa Ufaransa, Randal Kolo Muani kwenda Chelsea kama sehemu ya ofa ya kuipata saini ya straika wa Chelsea, Christopher Nkunku mwisho wa msimu huu. Nkuku sio mmoja kati ya wachezaji wanaopata nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Chelsea hali inayosababisha atamani kuondoka. Mkataba wake unamalizika mwaka 2029 ingawa Kocha wake, Enzo Maresca anadai bado ana mipango naye.


CRYSTAL Palace ni miongoni mwa timu zinazohitaji saini ya beki wa Lecce na timu ya taifa ya  Denmark, Patrick Dorgu, 20, ambaye anawindwa na timu mbalimbali barani Ulaya. Maskaut kutoka timu mbalimbali wamekuwa wakihudhuria mechi za Lecce kwa ajili ya kumtazama Dorgu ambaye msimu huu amecheza mechi 14 za michuano yote na kufunga mabao matatu.


RIPOTI zinadai Manchester United ipo tayari kumuuza straika wao, Marcus Rashford katika dirisha la majira ya kiangazi mwakani. Rashford mwenye umri wa miaka 27, haonekani kuwa katika mipango  ya kocha wa sasa wa timu hiyo Ruben Amorim. Msimu huu amecheza mechi 20 za michuano yote na kufunga mabao matano na pamoja na kutarajiwa angekuwa mmoja wa nyota tishio kwenye kikosi hicho lakini ameshindwa kuonyesha makali.


REAL  Betis inataka kumsajili kiungo Real Madrid, Dani Ceballos, 28, dirisha la majira ya baridi mwakani na tayari imeshaanza mazungumzo naye. Ceballos ambaye hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Madrid, mkataba wake na wababe hao unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu huu amecheza mechi nane za michuano yote.


LIVERPOOL imeanza mazungumzo na wawakilishi wa beki wa  Bayer Leverkusen, Jeremie Frimpong, 23, ili kumsajili dirisha la majira ya kiangazi mwakani kwa ajili ya kuziba pengo la Trent Alexander-Arnold, 26, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu na hadi sasa hawajafikia makubaliano ya kumuongeza.


MANCHESTER United haina mpango wa kumpa ofa ya mkataba mpya kiungo wao raia wa Denmark, Christian Eriksen, 32, mwisho wa msimu huu pale mkataba wake utakapomalizika. Eriksen mwenye ambaye aliwahi kuhusishwa kuondoka mwisho wa msimu uliopita, msimu uliopita alicheza mechi 14 za michuano yote na kufunga mabao manne.