Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Che Malone aendeleza kuvuna mataji Algeria

Muktasari:

  • Mlinzi huyo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha USM Alger, akichangia mafanikio ya klabu hiyo katika mashindano ya ndani na ya kimataifa.

Beki wa zamani wa Simba na timu ya Cameroon, Che Malone Fondoh (27) anaendelea kuimarisha rekodi yake ya mafanikio katika soka la Afrika, akivuna mataji na tuzo mbalimbali akiwa na klabu yake ya USM Alger ya Algeria.

Mlinzi huyo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha USM Alger, akichangia mafanikio ya klabu hiyo katika mashindano ya ndani na ya kimataifa.

Miongoni mwa mafanikio yake ni kutwaa Kombe la Algeria mwaka 2026, baada ya USM Alger kuichapa CR Belouizdad mabao 2-1 katika mchezo wa fainali.

Mbali na mafanikio ya timu, Fondoh pia ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Kigeni nchini Algeria, iliyotolewa Mei 12, 2026, ikiwa ni heshima inayotambua mchango wake katika soka la nchi hiyo.

Katika mashindano ya kimataifa, jina la Fondoh limehusishwa pia na mafanikio ya USM Alger ya kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2025/26.

Mafanikio hayo yameongezewa na ubingwa wa CAF Super Cup, baada ya USM Alger kuichapa Mamelodi Sundowns mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa jana.

Mfululizo huo wa mafanikio unaendelea kuimarisha nafasi ya Fondoh katika kikosi cha USM Alger, huku beki huyo akiendelea kujijengea jina katika medani ya soka la Afrika.