Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bato la Ulaya kumekucha EPL!

BATO Pict
BATO Pict

Muktasari:

  • Mabingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, Liverpool imeshajihakikishia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, wakati Arsenal baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle United umewafanya kukamatia tiketi ya kucheza michuano hiyo ya Ulaya msimu ujao.

LONDON, ENGLAND: MBIO za ubingwa wa Ligi Kuu England zimeshakwisha. Vita ya kushuka daraja, imeshakwisha. Lakini, ukiweka kando vita ya kusaka Kiatu cha Dhahabu, iliyobaki ni ile ya kuwania tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na  sasa shughuli hadi mwisho wa msimu.

Mabingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, Liverpool imeshajihakikishia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, wakati Arsenal baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle United umewafanya kukamatia tiketi ya kucheza michuano hiyo ya Ulaya msimu ujao.

Sasa vita imebaki kwa Newcastle, Chelsea, Aston Villa, Manchester United na Nottingham Forest kwenye kuwania nafasi tatu zilizobaki za kucheza ligi hiyo msimu ujao.

Man City inashika namba sita kwenye msimamo wa ligi, lakini imecheza mechi chache ukilinganisha na wapinzani wao wengine kwenye mbio hizo za kusaka tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Man City sasa itahitaji kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Bournemouth uwanjani Etihad, Jumanne na itapata nafasi ya kupanda hadi nafasi ya tatu, pointi 68.

Newcastle, Chelsea na Aston Villa zimefungana kila mmoja ikiwa na pointi 66.

Wastani mzuri wa tofauti ya mabao unawaweka pazuri Newcastle mbele ya Chelsea, wakati Aston Villa imeachwa nyuma kwa mabao 11 dhidi ya The Blues. Newcastle imeizidi mabao mawili Chelsea.

Forest yenyewe imeachwa nyuma pointi moja, ikimiliki 65, sawa za Man City kwa sasa, lakini wameachwa nyuma kutokana na tofauti ya mabao. Kama Man City itaichapa Bournemouth, kisha ikienda kushinda dhidi ya Fulham kwenye mechi yao ya mwisho wa msimu, itakuwa imejihakikishia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na hivyo itakuwamo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Newcastle itakuwa St James' Park kumalizana na Everton, Jumapili na uhakika wao wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya utapatikana kwa kushinda tu katika mechi hiyo.

Chelsea itakuwa na mechi inayohitaji ujanja mwingine kutoboa, kutokana na kukumbana na Nottingham Forest, ambayo pia ipo kwenye mbio za kusaka tiketi ya michuano hiyo. Hiyo ni mechi ya kufa, kupona kwa miamba ya The Blues dhidi ya Forest, ambayo itapigwa uwanjani The City Ground.

Katika mchezo huo, Kocha Enzo Maresca wa Chelsea atalazimika kupambana asipoteze mbele ya Forest ya Kocha Nuno Espirito Santo ili kuendelea kuwa juu yao. Kama mechi hiyo ya City Ground ikimalizika kwa sare, Aston Villa itakuwa juu kwenye msimamo wa ligi endapo kama kikosi hicho cha Kocha Unai Emery kitaichapa Manchester United uwanjani Old Trafford.

Ili kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, Forest itahitaji kuichapa Chelsea huku ikiombea moja ya kati ya Newcastle au Aston Villa isipate ushindi katika mechi zao za mwisho za mwisho wa msimu, au Man City isishinde mechi zao mbili zilizobaki.

Kwenye mchakato huo, timu itakayoshika nafasi ya sita itafuzu kucheza Europa League.

Kama Chelsea itaangukia kwenye nafasi ya sita, timu itakayoshika nafasi ya saba pia itapata nafasi ya kucheza michuano ya Europa League - kama The Blues itabeba taji la Conference League.

Timu sita zitaiwakilisha England kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Hiyo inatokana na kuwa na timu mbili zilizotinga fainali ya Europa League msimu huu, Tottenham na Man United na timu itakayoshinda kwenye mechi ya fainali Jumatano, itakamatia tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.


MSIMAMO WA MBIO ZA KUSAKA TIKETI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA

                               P        W      D      L       F       A       GD   Pts

3. Newcastle       37      20      6        11      68      46      +22   66

4. Chelsea            37      19      9        9        63      43      +20   66

5. Aston Villa        37      19      9        9        58      49      +9     66

6. Man City            36      19      8        9        67      43      +24   65

7. Nottm Forest     37      19      8        10      58      45      +13   65