Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca yaziibukia Liverpool, Madrid dili la Marc Guehi

Muktasari:

  • Awali Liverpool na Real Madrid ndizo zilitajwa kuonyesha nia ya kumsajili beki huyo ambaye amekuwa mhimili muhimu katika safu ya ulinzi ya Palace.

BARCELONA ipo tayari kuingia kwenye vita dhidi ya Liverpool na Real Madrid kwa ajili ya kuipata saini ya beki kisiki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi, 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo atakuwa mchezaji huru.

Awali Liverpool na Real Madrid ndizo zilitajwa kuonyesha nia ya kumsajili beki huyo ambaye amekuwa mhimili muhimu katika safu ya ulinzi ya Palace.

Guehi amecheza takriban mechi 90 za Ligi Kuu England tangu ajiunge na Palace 2021 akitokea Chelsea kwa dau la Pauni 18 milioni.

Liverpool ilikuwa karibu kuipata huduma ya staa huyo kwa ada ya Pauni 35 milioni katika dirisha lililopita na ilishamfanyia hadi vipimo vya afya kabla ya mambo kuharibika baada ya kocha wa Palace kutishia kujiuzuru ikiwa angeuzwa.

Barca inataka kumsajili kwa usajili huru pekee na haitajaribu kuingia katika vita yoyote Januari mwakani ambapo Madrid pamoja na Liverpool zinapiga hesabu kuwasilisha ofa kwa ajili ya kuipata huduma ya fundi huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.


Joe Gomez

BEKI wa Liverpool na England, Joe Gomez alikuwa karibu kutua Crystal Palace au Brighton katika siku ya mwisho ya dirisha lililopita usajili, lakini alibaki Anfield baada ya Liverpool kushindwa kukamilisha usajili wa Marc Guehi. Gomez mwenye umri wa miaka 28, ameichezea Liverpool zaidi ya mechi 200, akiwa sehemu ya kikosi kilichoshinda taji ka EPL kwa mara kwanza baada ya miaka 30 chini ya Jurgen Klopp.


James Tarkowski

EVERTON inatathmini wachezaji watatu ambao ni beki wa kati James Tarkowski, 31; beki wa kushoto Vitalii Mykolenko, 26 pamoja na James Garner, 24, ambaye ni kiungo wa England aliyewahi kuichezea Manchester United hapo awali. Mastaa hao wanatarajiwa kumaliza mikataba mwisho wa msimu huu na Everton inafanya majadiliano ili kuamua ikiwa itawasainisha mikataba mipya au itawaacha waende ifikapo mwisho wa msimu.


Carlos Baleba

MANCHESTER United huenda ikarudi tena katika mazungumzo na Brighton kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na timu ya taifa ya Cameroon, Carlos Baleba, 21, dirisha lijalo la majira ya baridi baada ya kushindwa kumsaini kwenye dirisha lililopita. Baleba alisajiliwa na Brighton kutoka Lille 2023 kwa ada ya Euro 27 milioni na tangu wakati huo ameonyesha kiwango bora kilichovutia vigogo mbalimbali barani Ulaya.


Emiliano Martinez

Kipa wa Aston Villa na timu ya taifa ya Argentina, Emiliano Martinez, 33, amerejeshwa kwenye kikosi kwa ajili ya kukitumikia msimu huu baada ya kuwaambia mabosi kwamba hana mpango wa kwenda kucheza Saudi Arabia wala Uturuki ambako timu kadhaa zinataka kumsajili kufuatia dili la kujiunga na Manchester United kufeli siku ya mwisho ya dirisha lililopita la usajili. Kipa huyo ambaye ni bingwa wa Kombe la Dunia 2022, mkataba wake unamalizika 2029.


Jan Paul van Hecke

MPANGO wa Tottenham Hotspur kutaka kumsajili beki wa kati wa Brighton, Jan Paul van Hecke, 25, umezidi kuwa na matumaini baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi kugoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika kikosi hicho. Paul ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Brighton na amekataa kusaini mkataba mpya kwa sababu anataka chagamoto mpya sehemu nyingine.


Jesurun Rak-Sakyi

RANGERS ya Scotland huenda ikarudi tena na ofa mpya kwa ajili ya kumsajili winga wa Crystal Palace, Jesurun Rak-Sakyi mwenye umri wa miaka 22, baada ya ofa yao ya mwisho kukataliwa siku ya mwisho ya dirisha la usajili.

Jesurun ambaye hata yeye alitamani kuondoka ili kupata nafasi zaidi ya kucheza, anadaiwa alishakubaliana na Rangers juu ya masuala ya mshahara na kilichokuwa kinasubiriwa ni timu hiyo kufikia makubaliano na Palace.


Sasa Kalajdzic

LICHA ya kumruhusu mshambuliaji Sasa Kalajdzic kujiunga na LASK, mabosi wa Wolves wanaweza kumrudisha staa huyu wa kimataifa wa Austria ifikapo Januari mwakani ikiwa watataka kufanya hivyo. Katika mkataba wa makubaliano ya uhamisho wa mkopo timu hizo mbili zimeweka kipengele hicho kinachomruhusu Sasa mwenye umri wa miaka 28 kurudi na hakuna kipengele kinachoipa nguvu LASK ya kumsainisha mkataba wa kudumu.