Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca yaanza mazungumzo ya kumsajili Julian Alvarez

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Álvarez ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao na kucheza katika mifumo tofauti ya ushambuliaji, jambo linalomfanya kuwa chaguo linalovutia kwa Barcelona inayotaka kuongeza katika safu yao ya ushambuliaji.

BARCELONA imeanza mawasiliano na Atletico Madrid ili kujua msimamo wao kuhusu uwezekano wa kuwauzia  mshambuliaji wao wa kimataifa wa Argentina, Julian Alvarez, 26, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Álvarez ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao na kucheza katika mifumo tofauti ya ushambuliaji, jambo linalomfanya kuwa chaguo linalovutia kwa Barcelona inayotaka kuongeza katika safu yao ya ushambuliaji.

Hata hivyo, dili hilo linaweza kuwa gumu kutokana na umuhimu wa mchezaji huyo katika kikosi cha Atletico ambayo hadi sasa haijaweka wazi ikiwa itakuwa tayari kumuuza au laa.

Mbali na Barca, staa huyu pia huduma yake imekuwa ikinyemelewa kwa muda mrefu na Arsenal ambayo ilianza mazungumzo na wawakilishi wake tangu dirisha la majira ya baridi mwaka huu.

Msimu huu, Alvarez amecheza mechi 47 za michuano yote, amefunga mabao 19  na kutoa asisti tisa. Mkataba wake unamalizika mwaka 2030.


Liam Delap

MSHAMBULIAJI wa Chelsea na England, Liam Delap, 23, anataka kuendelea  kubaki katika klabu hiyo na kupigania nafasi yake katika kikosi cha kwanza baada ya kukumbana na changamoto ya majeraha tangu asajiliwe msimu huu.

Chelsea inatarajiwa kufanya maamuzi makubwa kuhusu washambuliaji wao katika dirisha la majira ya kiangazi, jambo linaloweza kuathiri nafasi ya Delap.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2031, kuna ripoti zinazodai kwamba anaweza akatolewa kwa mkopo.


Jadon Sancho

BORUSSIA Dortmund inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili tena winga wa Manchester United, Jadon Sancho, 26, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hata hivyo, ripoti zinadai wanakutana na upinzani kutoka kwa Aston Villa ambayo inataka kumsajili mchezaji huyo atakapokuwa  huru Julai mwaka huu.

Sancho amewahi kuwa na mafanikio akiwa Dortmund kabla ya kuondoka, jambo linalofanya mabosi wa klabu hiyo kuamini atasaidia kikosi chao.


Yoane Wissa

NEWCASTLE United inadaiwa kuwa katika mpango wa kumuuza mshambuliaji wao, Yoane Wissa, 29, dirisha lijalo ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu imsajili.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, Newcastle inahitaji Pauni 50 milioni ili kumuuza Wissa ikiwa ni sehemu ya mikakati yao ya kusuka upya safu ya ushambuliaji.

Klabu nyingi zinaonekana kuvutiwa na staa huyu na ikiwa ataweka rasmi sokoni huenda bei yake ikapanda zaidi kutokana na kugombaniwa.


Yan Diomande

LIVERPOOL inaweza kukosa nafasi ya kumsajili winga wa RB Leipzig, Yan Diomande, 19, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa moja kati ya sababu zinazodaiwa kuchangia Liverpool kuwa katika hatari ya kumkosa fundi huyo ni Leipzig haitaki kumwachia kwa sasa, walau acheze kwa msimu mmoja zaidi kabla ya kumruhusu kuondoka.

Vigogo wa Leipzig wanaamini ikiwa Diomande ataendelea kusalia katika kikosi chao kwa mwaka mmoja zaidi.


Harry Kane

BAYERN Munich inatarajiwa kuanza mazungumzo ya kumwongeza mkataba mshambuliaji wao, Harry Kane, 32, mwisho wa msimu huu.

Mabingwa hao wa Ujerumani wanataka kuongeza muda wa Kane kubaki kwa miaka miwili zaidi kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu ajiunge nao.

Kane ameendelea kuwa tegemeo kubwa katika safu ya ushambuliaji ya Bayern, msimu huu amefunga mabao 53 katika mechi 45 za michuano yote.


Dusan Vlahovic

AC Milan na Bayern Munich zimeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus, Dusan Vlahovic, 26, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hatma ya Vlahovic Juventus inaonekana kutegemeana na mazungumzo ya mkataba mpya na klabu hiyo ambayo yanaendelea kwa sasa. Ikiwa hakutokuwa na makubaliano, Juventus itamuuza dirisha lijalo ili kuepuka kumpoteza bila ya kupata chochote.


Zeki Celik

LIVERPOOL imepiga hatua kubwa katika mazungumzo yao ya  kumsajili beki wa AS Roma na timu ya taifa ya Uturuki Zeki Celik mwenye umri wa miaka 29, ambaye wakala wake ameweka wazi kuwa  mchezaji huyo anataka kutafuta changamoto mpya nje ya Italia kwa msimu ujao.

Inaelezwa Liverpool wanamwona Celik kama chaguo sahihi la kuongeza ushindani katika upande wa kulia wa safu yao ya ulinzi.