Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Balaa la kadi ya Ronaldo

Muktasari:

  • Ronaldo, 40, ambaye alionyeshwa kadi nyekundu ya kwanza katika miaka yake 22 aliyocheza soka la kimataifa akiwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno, ilikuja baada ya mechi ya kichapo cha kushtua huko Dublin.

LISBON, URENO: SUPASTAA, Cristiano Ronaldo kijasho kinamtoka kwa sasa juu ya uwezekano wa kukutana na adhabu ambayo inaweza kumfanya akose mechi mbili za kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.

Ronaldo, 40, ambaye alionyeshwa kadi nyekundu ya kwanza katika miaka yake 22 aliyocheza soka la kimataifa akiwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno, ilikuja baada ya mechi ya kichapo cha kushtua huko Dublin.

Na adhabu hiyo inakuja katika kipindi ambacho Ronaldo amebainisha kwamba fainali hizo za Kombe la Dunia 2026 zitakuwa fainali zake za mwisho kwenye mchezo wa soka. Awali, Ronaldo alionyeshwa kadi ya njano baada ya tukio lililotokea ndani ya penalti boksi kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Ireland, Dara O’Shea.

Kadi hiyo ya njano baadaye ilibadilishwa na mwamuzi wa Sweden, Glenn Nyberg baada ya kwenda kuangalia marudio ya picha kwenye VAR, hivyo Ronaldo alitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu kutokana na kiwiko hicho alichompiga beki wa kati wa Ipswich.

Ronaldo atakosa mechi ya Jumapili ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Armenia huko Oporto, ambapo pointi moja tu kwa Ureno itawapa nafasi ya kufuzu michuano hiyo kwa kuongoza kundi lake na hapo kikosi hicho cha kocha Roberto Martinez kutakwenda Marekani, Canada na Mexico.

Lakini, mbele ya kamati ya nidhamu ya Fifa, adhabu inaweza kuwa mara mbili yake na kuna wasiwasi Ronaldo anaweza kufungiwa mechi tatu.

Wakati mechi za kufuzu kwa upande wa Ulaya zikisimamiwa na Uefa, kanuni ya nidhanu za Fifa zinafanya kazi kwenye fainali za Kombe la Dunia na inachosema ni kwamba adhabu inaweza kuwa mechi mbili kutokana na ukubwa wa faulo iliyofanyika.

Na zaidi, kwenye kosa alilofanya supastaa huyo wa Ureno, kanuni zinafichua kwamba adhabu inaweza kuwa walau mechi tatu, endapo kama itakuwa ni tukio la unyanyasaji, kupiga kiwiko, kupiga ngumi, kupiga teke, kutemea mate au kumpiga mpinzani.

Kutokana na hilo, kama Ureno itafuzu Jumapili, Ronaldo anaweza kujikuta akikosa mechi mbili za kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia.

Kwa sababu hatua ya makundi inahusisha mechi tatu kwenye Kombe la Dunia, Ronaldo anaweza kuishia kucheza mechi moja tu kama Ureno itashindwa kuvuka hatua ya 32 bora.

Kinyume cha hapo, endapo kama Ureno itashindwa kufuzu moja kwa moja Jumapili, hivyo, Ronaldo atakuwa nje kwenye mechi ya mchujo itakayofanyika Machi mwakani.

Kocha wa Ureno, Martinez alisema watapambana endapo kama kutakuwa na mpango wowote wa kumwongezea adhabu supastaa wao huyo.

Mwaka 2012, Chama cha soka cha England (FA) kiliiomba Uefa kumpunguzia adhabu Wayne Rooney kuwa mechi mbili baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mechi ya kufuzu dhidi ya Montenegro, hivyo kumruhusu mchezaji mwenza wa zamani wa Ronaldo, Rooney kupata nafasi ya kufunga bao la ushindi la England kwenye mechi ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Ukraine.

Martinez alisema: “Cristiano hajawahi kutolewa uwanjani kwa kadi nyekundu katika mechi 226. Hii inaumiza. Alikuwa na dakika 60 au 58 za kuvutwavutwa kwenye boksi, kusukumwa na alikuwa akijaribu kujiondoa kwa yule beki, ambaye alijiangusha na kuigiza kama amepigwa na Ronaldo. Tumekubali uamuzi wa kadi nyekundu. Sitaki kusema vitu vingine, lakini kwa tukio lile linaonekana kama vile mwamuzi alihamasishwa.”

Wakati kadi nyekundu hiyo ikiwa ya kwanza kwa Ronaldo kwenye soka la timu ya taifa, huko kwenye klabu alikula umeme mara 12, hivyo kuwa na jumla ya kadi 13 nyekundu katika maisha yake yote ya soka.