Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta adai sekunde 10 tu zimetosha kwa Sterling

Muktasari:


  • Sterling, 29, alijiunga na Arsenal kwa mkopo akitokea Chelsea kwenye saa za mwisho kabisa za kufungwa kwa dirisha la usajili mwezi uliopita baada ya kuambiwa bayana na kocha Enzo Maresca kwamba hatapata nafasi ya kucheza akiendelea kubaki Stamford Bridge.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema imemchukua sekunde 10 tu kushawishika juu ya kumsajili Raheem Sterling kwa sababu ameona kiu ya kutaka mafanikio inavyomkereketa staa huyo wa zamani wa Chelsea.

Sterling, 29, alijiunga na Arsenal kwa mkopo akitokea Chelsea kwenye saa za mwisho kabisa za kufungwa kwa dirisha la usajili mwezi uliopita baada ya kuambiwa bayana na kocha Enzo Maresca kwamba hatapata nafasi ya kucheza akiendelea kubaki Stamford Bridge.

Sterling na Arteta walizungumza kwenye simu na hapo kocha huyo Mhispaniola alipata majibu kwamba mchezaji huyo atakwenda kuwa mtu sahihi kwenye kikosi chake. Lakini, wawili hao walikuwa pamoja pia huko Manchester City, wakati Arteta alipokuwa msaidizi wa Pep Guardiola.

Na sasa wamekutana tena huko Arsenal na hapo Arteta alisema: "Simu ya kwanza tu nilipompigia, nilijua ndani ya sekunde 10 tu za kwanza kwamba tunahitaji kumsajili na yeye alionyesha dhamira ya kuja kwetu. Sekunde 10 tu nilijua kila kitu kabla sijamuuliza swali jingine.

"Niliona ana njaa. Ni mchezaji anayetaka kucheza kila dakika kwenye kila mechi. Unaliona hilo, ni safi kuwa naye. Atatufanya kuwa bora."

Sterling anatarajia kucheza mechi yake ya kwanza Arsenal leo Jumapili kwenye kipute cha North London Derby huko Tottenham. Arteta atahitaji huduma bora kutoka kwa staa huyo wa zamani wa Liverpool kwenye mechi hiyo ya mahasimu wao kwenye Ligi Kuu England, Spurs.


MISHAHARAN MIKUBWA ARSENAL

1.Raheem Sterling, Pauni 325,000 kwa wiki

2.Kai Havertz, Pauni 280,000 kwa wiki

3.Gabriel Jesus, Pauni 265,000 kwa wiki

4.Declan Rice, Pauni 240,000 kwa wiki

5.Martin Odegaard, Pauni 240,000 kwa wiki

6.Thomas Partey, Pauni 200,000 kwa wiki