Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Algeria yaanza kwa ushindi WAFCON

Muktasari:

  • WAFCON iliyopita mechi ya kwanza ya ufunguzi dakika 90 zilitamatika kwa sare ya 2-2 iliyowakutanisha Morocco dhidi ya Zambia moja kati ya mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa.

ALGERIA imeandika historia ya kuanza ufunguzi wa mechi ya kwanza ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afika kwa Wanawake WAFCON kwa ushindi ikiitandika Senegal mabao 2-0 kwenye mechi ya kundi A.

WAFCON iliyopita mechi ya kwanza ya ufunguzi dakika 90 zilitamatika kwa sare ya 2-2 iliyowakutanisha Morocco dhidi ya Zambia moja kati ya mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo huo uliopigwa  kwenye Uwanja wa Olympic mjini Rabat, Morocco yanapofanyika mashindano hayo kwa mwaka huu, ambapo Algeria ilipata mabao yake kupitia kwa Marine Dafeur aliyefunga kwa penalti dakika ya 42 na Melissa Bethi aliyefunga bao la pili dakika ya 88 na kuipa Algeria pointi tatu za kwanza za Kundi A.

Algeria ilionyesha nidhamu ya hali ya juu licha ya kuiachia Senegal umiliki wa mpira kwa asilimia 53.6 dhidi ya 46.4. Hata hivyo, ubora wao katika kutumia nafasi ulifanya tofauti, wakipiga mashuti matano yaliyolenga lango na kufunga mabao mawili yaliyowapa pointi tatu muhimu.

Bao la kwanza lilipatikana dakika ya 42 kupitia Marine Dafeur, aliyefunga kwa utulivu  mkwaju huo wa penalti na kuipeleka Algeria kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0. Senegal ilijaribu kurejea kipindi cha pili, lakini ilishindwa kupenya safu ya ulinzi ya Algeria iliyokuwa imara muda wote wa mchezo.

Senegal ilitengeneza mashambulizi kadhaa na kupiga mashuti 11, mawili pekee yakilenga lango. Kipa C. N'Gazi alikuwa makini langoni kwa kuokoa michomo miwili muhimu, huku safu ya ulinzi iliyoongozwa na M. Belkhite ikidhibiti vizuri washambuliaji wa wapinzani.

Dakika ya 88, Melissa Bethi alizima matarajio ya Senegal kusawazisha bao, baada ya kuongeza bao la pili.

Takwimu za mchezo huo zinaonyesha, Algeria ilipiga mashuti 10 dhidi ya 11 ya Senegal, lakini ililenga lango mara tano huku Senegal ikifanya hivyo mara mbili.

Senegal pia ilifanya makosa 19 dhidi ya 11 ya Algeria na kuonyeshwa kadi tatu za njano, jambo lililoonyesha ilivyolazimika kutumia nguvu nyingi kuzuia mashambulizi ya wapinzani wake.

Ushindi huo unaipa Algeria nafasi nzuri ya kujiweka vizuri kwenye mechi ifuatayo dhidi ya wenyeji Morocco.