Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Al Hilal yaichapa Tusker

MTASINGWA Pict

Muktasari:

  • Ushindi huo umeifanya Al Hilal kuweka mazingira mazuri ya kutinga nusu fainali, huku Tusker ikianza vibaya michuano hiyo tofauti na wakenya wenzao, Gor Mahia ambao waliichapa APR ya Rwanda mabao 5-0.

AL Hilal Omdurman ya Sudan, imeanza vizuri  michuano ya Kombe la CECAFA Kagame 2026 baada ya kuichapa Tusker FC ya Kenya mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi C uliochezwa leo Jumapili Julai 26, 2026 kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, Rwanda.

Ushindi huo umeifanya Al Hilal kuweka mazingira mazuri ya kutinga nusu fainali, huku Tusker ikianza vibaya michuano hiyo tofauti na wakenya wenzao, Gor Mahia ambao waliichapa APR ya Rwanda mabao 5-0.

Al Hilal ilianza mchezo  huo kwa kasi na kutengeneza nafasi kadhaa kabla ya kupata bao la kuongoza dakika ya 30 kupitia Mamudu Karamadini.

Kipindi cha kwanza kilimalizika Al Hilal ikiwa mbele kwa bao 1-0 huku Tusker ikishindwa kutumia nafasi chache ilizozipata kutikisa nyavu.

Kipindi cha pili kilikuwa na ushindani mkubwa ambapo Tusker iliongeza kasi kutafuta bao la kusawazisha, lakini safu ya ulinzi ya Al Hilal ikiongozwa na kipa wa zamani wa Azam, Mohamed Mustafa ilisimama imara na kuzuia mashambulizi yote.

Wakati Tusker ikipambana walau kupata  sare, Al Hilal ilitumia nafasi hiyo kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kufanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 90+5 kupitia  Salim Adams, aliyefunga kwa shuti kali na kuhitimisha matumaini ya wapinzani wao.

Matokeo hayo yanaifanya Al Hilal kuongoza muda kundi C ikiwa na pointi tatu na mabao mawili ya kufunga bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa, huku Tusker ikilazimika kupambana katika michezo miwili iliyosalia ili kufufua matumaini ya kufuzu nusu fainali.

Michuano hiyo inayoshirikisha timu 12 zilizopangwa kwenye makundi matatu, kinara wa kila kundi atafuzu nusu fainali, kisha itaangaliwa timu moja itakayomaliza nafasi ya pili ikiwa na matokeo bora zaidi ya nyingine nayo kufuzu nusu fainali kukamilisha idadi ya timu nne zitakazoendelea na safari ya kuwania ubingwa unaoshikiliwa na Singida Black Stars.