AEK Larnaca yaishangaza Crystal Palace, Fiorentina yatembeza dozi
Muktasari:
- Jean-Philippe Mateta alipiga mpira uliogonga mwamba na kupoteza nafasi nyingine kwa kichwa katika kipindi cha kwanza kwa upande wa wenyeji.
Mechi ya nyumbani kwa Crystal Palace kwenye hatua ya makundi ya UEFA Conference League haikuenda kama walivyotarajia, huku Edin Džeko akiweka rekodi katika ushindi wa Fiorentina, mitanange hiyo ikipigwa usiku wa Oktoba 23, 2025.
CRYSTAL PALACE 0-1 AEK LARNACA
AEK Larnaca imeonesha ujasiri mkubwa baada ya bao kali la Riad Bajić na uchezaji wa kiwango cha juu wa kipa Zlatan Alomerović kuwapa ushindi wa kushangaza jijini London.
Jean-Philippe Mateta alipiga mpira uliogonga mwamba na kupoteza nafasi nyingine kwa kichwa katika kipindi cha kwanza kwa upande wa wenyeji.
Timu ya Cyprus ilitumia vizuri fursa adimu walipopata, ambapo Bajić alipiga shuti kali na kutikisa nyavu dakika ya 51.
Alomerović kisha alifanya uokoaji wa kipekee kuzuia shuti jingine la Mateta, na kufanya mechi ya kwanza ya Palace nyumbani kwenye michuano ya Ulaya kumalizika kwa kichapo.
SK RAPID 0-3 FIORENTINA
Akiwa na umri wa miaka 39 na siku 220, Edin Džeko amekua mfungaji mkongwe zaidi katika historia ya UEFA Conference League, baada ya kutupia wavuni pasi ya Niccolò Fortini muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza mjini Vienna. Cher Ndour aliwapa Fiorentina uongozi dakika ya tisa baada ya kuunganisha mpira uliorudishwa na kipa Niklas Hedl kufuatia shuti la Džeko.
Baada ya bao la Džeko ambalo lilikuwa lake la 67 katika mashindano ya klabu vya Ulaya, Albert Gudmundsson alifunga bao la tatu mwishoni kukamilisha ushindi wa pili mfululizo kwa kikosi cha Stefano Pioli.
MATOKEO
AEK Athens 6-0 Aberdeen
Häcken 2-2 Rayo Vallecano
Breidablik 0-0 KuPS Kuopio
Shakhtar Donetsk 1-2 Legia Warszawa
Drita 1-1 Omonoia
Rijeka p-p Sparta Praha
Shkëndija 1-0 Shelbourne
Strasbourg 1-1 Jagiellonia Białystok
SK Rapid 0-3 Fiorentina
Mainz 1-0 Zrinjski
AZ Alkmaar 1-0 Slovan Bratislava
Crystal Palace 0-1 AEK Larnaca
Hamrun Spartans 0-1 Lausanne-Sport
Lincoln Red Imps 2-1 Lech Poznań
Samsunspor 3-0 Dynamo Kyiv
Shamrock Rovers 0-2 Celje
Sigma Olomouc 1-1 Raków
Universitatea Craiova 1-1 Noah