Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shikangwa, Corazone kubaki Bongo

IMETIBUKA maze! Ile mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya timu ya taifa ya wanawake, Harambee Starlets, dhidi ya Albania iliyokuwa imepangwa kuchezwa Jumanne Aprili 11 mwaka huu jijini Tirana haipo tena.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF) iliyotumwa kwenye vyombo vya habari, gemu hiyo imeyeyuka kutokana na kile kilichodaiwa ‘changamoto za mipango ya kusafiri’.

“Uamuzi mchungu umefikiwa kutokana na changamoto za usafiri ambazo zimesababisha kuwa na ugumu kufika Albania kabla ya April 11 licha ya juhudi za pamoja kutoka kwa wahusika wote,” ilisomeka taarifa hiyo.

Hata hivyo FKF bado imedhamiria mikakati mikubwa ya maendeleo ya soka nchini Kenya na ipo kwenye mazungumzo na nchi zingine kwa lengo la kupata mechi ya kirafiki kwa ajili ya Starlets.

Kulikuwa na tetesi Harambee Stars itacheza na majirani Tanzania Jumapili Aprili 9 katika uwanja ambao ungetangazwa baadaye lakini hamna kipya hadi sasa kuhusiana na mechi hiyo.

Kuyeyuka kwa mechi hiyo kunamaanisha kuvunjwa kwa kambi ya Harambee Starlets iliyojumuisha wachezaji 33 ambao waliitwa katika kikosi cha awali na kocha mkuu Godfrey Oduor.

Kati ya wachezaji hao, 17 wanakipiga nje ya nchi miongoni mwao akiwa straika Jentrix Shikangwa, kiungo Vivian Corazone na beki Ruth Ingosi wote wakikipiga na mabingwa wa Ligi Kuu Wanawake Tanzania Bara, Simba Queens.

Wachezaji hawa wamekuwa muhimili wa Simba Queens inayopania kutetea ubingwa wa soka la wanawake Bongo na kutwaa tena taji la CECAFA ili kukipiga Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Simba Queens jana walishuka katika uga wa Jamhuri jijini Dodoma kuwakabili wenyeji Fountain Gate ambayo pia ina wachezaji kutoka Kenya kama vile Monica Chebet, Peris Oside na Nelly Kache.