Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Onyango asongezwa kwa wanaomtamani

BEKI wa zamani wa Gor Mahia na Western Stima ambaye kwasasa anakipiga na Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Joash Onyango, amekuwa gumzo hususan baada ya ratiba ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika kutoka.
Onyango ambaye mkataba wake na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu huu, amekuwa akihusishwa na kutua Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Utamu sasa unakuja baada ya Simba kupangwa kucheza na Orlando Pirates mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika mzunguko wa kwanza ukipigwa Aprili 17 mwaka huu Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam huku mchezo wa marudiano ukichezwa wiki moja baadaye jijini Johannesburg.
Onyango amekuwa katika kiwango bora tangu atue Simba akitokea Gor Mahia na amekuwa chaguo la kwanza kwenye safu ya ulinzi hivyo haishangazi kuona akihusishwa na Orlando Pirates.
Inadaiwa Pirates wamempa ofa nono ili ajiunge nao wakati Simba nao pia wanamshawishi abaki lakini anachotaka Onyango ni maboresho ya mkataba wake.
Endapo Onyango na Simba yake wataitoa Pirates, watafuzu nusu fainali na kucheza na mshindi kati ya Al Ittihad Tripoli dhidi Al Ahly Tripoli zote za nchini Libya.
Naye Brian Mandela Onyango ambaye anakipiga na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, wao watacheza mchezo wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro Atletico ya Angola huku mshindi wa jumla akivaana na mshindi kati ya CR Belouizdad ya Algeria dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.
Mandela anatarajiwa kurudi kwenye kikosi cha kwanza baada ya kukosekana mchezo wa mwisho hatua ya makundi Mamelodi Sundowns ikiifunga Al-Merrikh ya Sudan kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa dhidi ya Al Hilal pia ya Sudan.