Zahera amtetea Yondani
Kigali, Rwanda. Kocha mkuu wa Yanga amegoma kumlaumu nahodha wake Kelvin Yondani akisema bao walilofungwa lilitokana na hali mbaya ya mvua.
Zahera amesema Yondani hakuwa na kosa katika kukubali kupitwa na mfungaji wa bao pekee katika mchezo huo.
Amesema mfungaji wa bao hill alinufaika na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa mpira kupita katika maji na kumpiga chenga beki wake huyo.
Amesema kama isingekuwa mvua hiyo kubwa hata matokeo ya mchezo huo yangekuwa tofauti kutokana na Rayon haikuwa timu ya kutisha.