Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zahera akomaa na safu ya ulinzi

Muktasari:

Yanga imepoteza mechi mbili katika mashindano msimu huu huku safu yake ya ulinzi imeruhusu mabao manne katika mechi mbili.

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema akili yake sasa ni kuhakikisha wanafanya marekebisho makubwa katika safu yake ya ulinzi.

Zahera amesema mabeki wake wa kati na hata wale wa pembeni wamekuwa wakisababisha makosa yanayowaghalimu katika mechi zao mbili zilizopita.

Kocha huyo amesema kazi ya kuyafanyia kazi hayo imeshaanza na kwamba bado itaendelea kufanyika mpaka mambo yatakapokuwa sawa.

Amesema kama kweli wanataka kuchukua ubingwa msimu huu makosa ya kujipanga vyema yaliyofanyika katika mechi zao mbili yanatakiwa kuondolewa kwa haraka.

"Tumekuwa tunafanya makosa makubwa mabeki wa kati na hata wa pembeni wamekuwa wakitusababishia matatizo,'amesema Zahera.

"Tunafanya kazi sasa ya kuondoa kasoro hizo na tutaendelea na kazi hii, makosa kama haya hayatakiwi kutokwea mara kwa mara kwa timu inayotaka kuchukua ubingwa."