Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yampata mrithi wa Jeannine

MRITHI Pict

Muktasari:

  • Sandrine anatua Jangwani baada ya kuwa miongoni mwa washambuliaji walioonyesha kiwango bora katika ligi ya wanawake ya Rwanda akifunga mabao 10 na kuongoza kwenye orodha ya wapachikaji mabao, sambamba na kuwa sehemu ya kikosi cha She Amavubi.

INAELEZWA Yanga Princess iko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Rwanda, Mutuyimana Sandrine baada ya kumpa mkataba wa miaka mitatu akitokea Inyemera WFC ya nchini kwao.

Sandrine anatua Jangwani baada ya kuwa miongoni mwa washambuliaji walioonyesha kiwango bora katika ligi ya wanawake ya Rwanda akifunga mabao 10 na kuongoza kwenye orodha ya wapachikaji mabao, sambamba na kuwa sehemu ya kikosi cha She Amavubi.

Ikumbukwe kabla ya Yanga kukubaliana naye kumsajili alikuwa tayari yuko nchini kwa zaidi ya mwezi mmoja akifanya majaribio na mazoezi na Yanga Princess, huku benchi la ufundi likipima uwezo wake kabla ya kumpa rasmi dili la kuitumikia timu hiyo kwa misimu mitatu.

MRI 01

Inaelezwa kipindi alichokuwa anafanya mazoezi na Wananchi hao kocha wa Yanga, Edna Lema ‘Mourinho’ amevutiwa na uwezo wake wa kufumania nyavu.

MRI 02

Mutuyimana anasajili Yanga kuziba nafasi ya Mrwanda mwenzie Jeannine Mukandayisenga ambaye aliuzwa hivi karibuni kwenda Wuhan Jiangda WFC inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake China.