Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yamliilia Mama Fatma Karume

Muktasari:

  • Yanga imesema imepokea taarifa hiyo kwa huzuni kubwa, ikimtaja marehemu Mama Fatma Karume kuwa mmoja wa viongozi waliokuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya klabu hiyo.

Uongozi wa Yanga, umeeleza kusikitishwa na kifo cha Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa klabu hiyo, Mama Fatma Karume, aliyefariki dunia jana, Septemba 21, 2026.

Yanga imesema imepokea taarifa hiyo kwa huzuni kubwa, ikimtaja marehemu Mama Fatma Karume kuwa mmoja wa viongozi waliokuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya klabu hiyo.

Akizungumza kuhusu msiba huo, Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, amesema klabu hiyo imepoteza kiongozi mwenye busara, hekima na aliyekuwa na mapenzi makubwa kwa Yanga.

“Huu ni msiba mkubwa kwetu. Tumepoteza kiongozi mkubwa mwenye busara, hekima na mapenzi makubwa na klabu yetu”.

Ameongeza kuwa miongoni mwa mambo ambayo Yanga itamkumbuka nayo Mama Fatma Karume ni mchango wake katika upatikanaji wa ardhi yaliyojengwa makao makuu ya klabu hiyo, yaliyopo Jangwani, Dar es Salaam.

“Tutamkumbuka Mama yetu Fatma Karume kwa mengi mazuri aliyofanya ndani ya klabu yetu, ikiwemo upatikanaji wa ardhi ya jengo letu la makao makuu, Jangwani jijini Dar es Salaam,” amesema.

Hersi amesema kifo cha Mama Fatma Karume ni pigo kwa Yanga, akimtaja kama mwanachama na moja ya nembo muhimu za klabu hiyo.

“Hakika, tumempoteza mwanachama na moja ya nembo ya klabu hii,” aliongeza.

Kupitia taarifa yake, Yanga imetoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wadau wa michezo nchini Tanzania, huku ikiwaombea wapate nguvu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.

“Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Ameen,” ilisema katika sehemu ya taarifa ya klabu hiyo.