FA Cup Unguja kuendelea Novemba 9
Muktasari:
- Mashabiki wanasubiri kuona ni timu zipi zitakazovuka salama katika hatua hiyo na kuendelea na safari ya kuwania taji la FA Cup.
HATIMAYE, hatua ya 32 bora ya michuano ya Kombe la FA Cup kwa Kanda ya Unguja inatarajiwa kuchezwa Novemba 9, 2026 kwa michezo minne ya ufunguzi.
Hatua hiyo itachezwa kuanzia Novemba 9, 2026 hadi Novemba 12, 2026 huku michezo ikipangwa katika viwanja vya Mao A na Mao B kwa nyakati za saa 8 mchana na saa 10 jioni.
Jumla ya timu 32 zitashiriki katika hatua hiyo, huku timu 16 zitakazofanikiwa kushinda zikisonga mbele na nyingine 16 zikimaliza safari yao katika mashindano hayo.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni KMKM SC, ambayo imelichukua taji hilo mara mbili mfululizo, hivyo msimu huu itakuwa na kazi ya kulinda heshima yake na kuwania ubingwa kwa mara nyingine.
Katika michezo itakayochezwa Mao A, saa 8 mchana, Uhamiaji FC itakutana na Ranger Bulls, kabla ya Muungano Rangers kucheza dhidi ya JKU SC saa 10 jioni. Katika Uwanja wa Mao B, Villa FC itamenyana na Muembe Makumbi City FC saa 8 mchana, huku Sebleni United ikicheza na Raskazone FC saa 10 jioni. Michezo mingine ya kukamilisha hatua hiyo itazikutanisha Black Mamba na Zimamoto FC katika Mao A saa 8 mchana, kabla ya Nungwi City kucheza na Kitope United saa 10 jioni.
Katika Mao B, Scud FC itaonyeshana kazi na Kikungwi Star saa 8 mchana, huku mchezo wa saa 10 jioni ukihusisha timu zitakazotajwa kwenye ratiba rasmi ya mashindano.
Mashabiki wanasubiri kuona ni timu zipi zitakazovuka salama katika hatua hiyo na kuendelea na safari ya kuwania taji la FA Cup.