Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaingia Uhuru, kimya kimya!

Muktasari:

  • Ujio wa timu hizo mbili umekuwa miongoni mwa matukio yanayovuta hisia kabla ya pambano hilo kubwa la dabi, huku mashabiki wakisubiri kuona ni timu gani itakayomaliza dakika 90 ikiwa na tabasamu.

YANGA imewasili katika Uwanja wa Uhuru saa 5:24 jioni, dakika mbili kabla ya watani wao wa jadi, Simba, waliofika saa 5:26 jioni kuelekea Dabi ya Kariakoo inayopigwa leo saa 1:00 usiku.

Ujio wa timu hizo mbili umekuwa miongoni mwa matukio yanayovuta hisia kabla ya pambano hilo kubwa la dabi, huku mashabiki wakisubiri kuona ni timu gani itakayomaliza dakika 90 ikiwa na tabasamu.

Tofauti na ilivyozoeleka katika baadhi ya michezo mikubwa, Simba na Yanga hazikutumia mabasi rasmi ya timu zao kuwasili uwanjani, badala yake ziliingia kwa kutumia magari aina ya coaster.

Yanga ndiyo iliyotangulia kuwasili, ikitumia dakika chache kuingia katika eneo la uwanja huo kupitia geti kuu. Kikosi hicho kiliingia kwa haraka na kimya kimya, bila makelele makubwa na hata baadhi ya mashabiki hawakujua kama wamewasili.

Jambo lililowashangaza mashabiki ni namna Yanga ilivyoingia bila kuambatana na ving'ora vya polisi, tofauti na msafara wa Simba, ambao uliingia uwanjani ukiwa na ving'ora hivyo.

Simba, ambao ni wenyeji wa mchezo huo, waliwasili dakika mbili baada ya Yanga, saa 5:26 jioni.