Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga watua Zanzibar kuivaa MC Alger

Muktasari:

  • Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 10:00 jioni.

IDADI ya wachezaji 30 wa Yanga wamefika Visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya MC Alger ya Algeria.

Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 10:00 jioni.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema wanaamini kambi ya siku tatu itatosha kuwapa maandalizi mazuri kwa ajili ya mechi hiyo.

“Kikosi cha wachezaji jumla 30 kikijumlisha viongozi na maofisa wa benchi la ufundi, kipo njiani hivi sasa kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wetu wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema Kamwe.

Kamwe amesema kuwa viingilio katika mchezo huo ni Sh5,000, Sh10,000, Sh20,000 na Sh30,000,

Kamwe alisema kuna umuhimu mkubwa kwa mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanjani kuiunga mkono timu hiyo.

“Ili kuhakikisha tunashinda michezo yetu yote ya nyumbani ni lazima tujaze uwanja kwa kununua tiketi kwa wingi. Tusijiamini kupita kiasi na kuwaachia wachezaji jukumu hilo peke yao.

“Nao wanahitaji sapoti yetu, hamasa na nguvu kutoka kwa mashabiki ili kuwapa morali ya kufanya vizuri wanapoona wamejaa.

“Huu si mchezo wa kumwachia Aziz KI au Shalulile pekee yao. Kila Mwananchi ana jukumu la kuhakikisha uwanja unajaa,” amesema Kamwe.