Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, Simba watofautiana sakata la Fadlu

Muktasari:

  • Timu hiyo ilitangaza kumdai Davids kiasi cha Sh124 milioni kwa kosa la kuvunja mkataba wake na klabu hiyo kwa njia zisizo halali.

Simba imethibitisha kwamba imelipwa deni ambalo ilikuwa inamdai Kocha Mkuu mpya wa Yanga, Fadlu Davids.

Timu hiyo ilitangaza kumdai Davids kiasi cha Sh124 milioni kwa kosa la kuvunja mkataba wake na klabu hiyo kwa njia zisizo halali.

Davids aliachana na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita baada ya mchezo wa ugenini wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United nchini Botswana.

Fadlu Davids aliiongoza Simba katika msimu wa 2024/2025 na kuiongoza kufika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Baada ya mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini dhidi ya Gaborone United, Septemba 20, 2025, Davids alitangaza kuachana na Simba na siku chache baadaye akajiunga na Raja Casablanca ya Morocco.

Hata hivyo Simba ilipeleka malalamiko yake kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ikidai kocha huyo amevunja mkataba kiholela ambapo iliamriwa Fadlu Davids alipe fidia ya kiasi hicho cha fedha Sh124 milioni.

Oktoba mwaka huu, Simba ilirudi tena FIFA kushinikiza imbane Fadlu alipe deni hilo na shirikisho hilo liliandika barua kwenda kwa Kocha huyo na Simba ikiwataarifu juu ya uwepo wa kesi baina ya pande hizo kwa ajili kujadili suala hilo.

Mapema leo Jumatatu, Novemba 23, 2026 Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amethibitisha kulipwa fedha hizo.

“Tunapenda kuthibitisha kuwa tumepokea malipo ya deni letu kutoka kwa aliyekuwa Kocha wetu Fadlu Davids yeye pamoja na wasaidizi wake.

“Deni hilo limelipwa na mwajiri wake wa sasa. Tunapenda kujipongeza Simba Sports kwa kuwa na nguvu ya kisheria ya kudai deni letu na kulipwa kwa wakati,” amesema Ally.

Hata hivyo Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa hana taarifa hizo.

"Suala la kulipa deni la kocha wetu, Fadlu Davids hilo sina taarifa nalo na ikitokea vinginevyo nitaweka wazi, ila ndugu zangu nawaomba mumuulize kwanza aliyechapisha hizo taarifa kazipata wapi," amesema Kamwe.