Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania watamba kushinda NCBA Kenya

WATANZANIA Pict

Muktasari:

  • Wachezaji hao ni Abdallah Singano, Letesia Kapalia na Julius Mwinzani, ambao wamepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya NCBA Tanzania Golf Series.

WACHEZAJI watatu wa gofu wa Tanzania wanatarajiwa kuondoka nchini leo kwenda Nairobi, Kenya, kushiriki mashindano ya NCBA Golf Group Finale yatakayofanyika keshokutwa.

Wachezaji hao ni Abdallah Singano, Letesia Kapalia na Julius Mwinzani, ambao wamepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya NCBA Tanzania Golf Series.

Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Gilman Kasiga, alisema ana imani na uwezo wa wachezaji hao kufanya vizuri katika mashindano yatakayoshirikisha washiriki kutoka Kenya, Uganda na Rwanda.

Alisema wachezaji hao wamejiandaa vyema na wako tayari kupeperusha bendera ya Tanzania katika jukwaa hilo la kikanda.

“Sina wasiwasi na wachezaji wa Tanzania. Wote ni wakali na wana nia ya kufanya vizuri katika mashindano hayo,” alisema Kasiga wakati wa kuwakabidhi bendera ya taifa.

Aliongeza kuwa ushiriki huo utawapa nafasi ya kupima viwango vyao dhidi ya wachezaji wa mataifa mengine, kupata uzoefu na kujenga mahusiano yatakayosaidia maendeleo yao katika mchezo huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa NCBA Tanzania, Alex Martin Mziray alisema benki hiyo inajivunia kuwa sehemu ya safari za wachezaji hao kwa kuwawezesha kushiriki mashindano nje ya Tanzania.

“Katika NCBA, tunaamini dhamira ya kufikia mafanikio haina mipaka. Kuwadhamini washindi hawa watatu kushiriki mashindano ya Nairobi ni sehemu ya dhamira yetu ya kuamini uwezo wa watu na kuwapatia fursa za kusonga mbele katika kutimiza malengo yao. Hii ndiyo maana halisi ya Banking on Belief,” alisema Mziray.

Alisema mashindano ya NCBA Golf Series yanawezesha wachezaji kuendeleza vipaji vyao, kujifunza mbinu mpya na kujipima dhidi ya washindani wenye uzoefu tofauti.

Kwa upande wake, kiongozi wa timu hiyo, Abdallah Kingano, alisema  “Ninaishukuru NCBA kwa kutuamini na kutupatia nafasi ya kushindana na wachezaji kutoka nchi nyingine za Afrika Mashariki. Natarajia kujifunza mengi, kutoa ushindani mzuri na kuiwakilisha Tanzania kwa heshima,” alisema.

Letesia Kapalia alisema mashindano hayo yatakuwa fursa ya kupima uwezo wao na kujifunza kutoka kwa wachezaji wenye uzoefu wa mataifa mengine, pia utawasaidia kuboresha viwango vyao na kujenga mahusiano mapya yatakayochangia maendeleo ya mchezo wa gofu.

Mashindano ya NCBA Golf Series yamekuwa jukwaa la kuwaunganisha wachezaji wa kulipwa, wasio wa kulipwa na vijana, huku yakitoa fursa kwa washiriki kuonyesha vipaji vyao na kushiriki ya ngazi ya juu.

Kupitia udhamini huo, NCBA inaendeleza falsafa yake ya Banking on Belief – Empowering Ambition, inayolenga kuwawezesha watu kutimiza malengo yao kupitia fursa mbalimbali.