Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasudani wa Yanga CAF wapata kocha mpya

Wasudani wa Yanga CAF wapata kocha mpya

MPINZANI wa Yanga kwenye hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika, Zalan FC ya Sudan ya Kusini jana imemtambulisha kocha mpya Baping Alliab.
Alliab ambaye amewahi kuwa Kocha wa Al Hilal Wau Sudan Kusini na kubeba Kombe la Ligi ataiongoza Zalan kwenye mechi za Afrika ambapo mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Septemba 9 hadi 11 huku marudiano ikichezwa Septemba 16 mpaka 18.
Mshindi wa jumla baina ya klabu hizo atacheza na mshindi kati ya St.Georges ya Ethiopia na Al Hilal ya Sudan.
“Uongozi wa Zalan FC unathibitisha kumteua Baping Aliap kama kocha mkuu wa Zalan FC kwa kipindi cha mwaka mmoja (1) ikitegemea kumuongeza mkataba kutokana na kiwango timu itakachoonyesha,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.
Kocha huyo msimu uliopita alikuwa anakinoa kikosi cha Al Hilal Wau ambapo waliibuka Mabingwa wa Sudan Kusini.