Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapinzani wa Simba CAFCL, wamsimamisha kazi kocha mkuu

WAPINZANI Pict

Muktasari:

  • Hatua hiyo ya kushtua imekuja wakati klabu hiyo ikijiandaa na mchezo mkubwa wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAFCL) dhidi ya wawakilishi wa Tanzania, Simba SC.

Siku chache kabla ya kuanza kwa kampeni za michuano ya kimataifa, miamba ya soka nchini Malawi, klabu ya Mighty Wanderers FC, imetangaza kumsimamisha kazi kocha mkuu wa timu hiyo, Bob Mpinganjira.

Hatua hiyo ya kushtua imekuja wakati klabu hiyo ikijiandaa na mchezo mkubwa wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAFCL) dhidi ya wawakilishi wa Tanzania, Simba SC.

Uamuzi huo wa bodi ya wakurugenzi ya Mighty Wanderers umechukuliwa saa chache baada ya timu hiyo kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ekhaya FC, katika mchezo wa fainali wa Kombe la Airtel Top 8 uliopigwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa Bingu. Kipigo hicho kimeacha simanzi kwa mashabiki na viongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake jijini Blantyre, hali iliyochochea mabadiliko ya haraka kwenye benchi la ufundi.

WAPI 02

Ili kuziba pengo hilo kuelekea mechi dhidi ya Simba SC, uongozi wa Wanderers umemtangaza aliyekuwa kocha msaidizi, MacDonald Nginde Mtetemera, kukimu nafasi hiyo kwa muda.

Katika hatua nyingine, klabu hiyo imemtangaza aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Malawi ( The Flames) na aliyewahi kuhudumu kama kocha msaidizi wa Yanga SC ya Tanzania, Patrick Mabedi, ndiye atakuwa Mshauri wa Benchi la Ufundi.

Uzoefu wa Mabedi katika soka la ukanda wa Afrika Mashariki, hususan nchini Tanzania, unatazamwa kama silaha muhimu itakayosaidia kuwapa mbinu Mighty Wanderers watakapoikabili presha ya kukutana na Simba SC.

WAPI 03

Mighty Wanderers inatarajiwa kuanza maandalizi ya mechi hiyo leo Jumatatu, Agosti 31, 2026, huku mechi ya mkondo wa kwanza ikipangwa kupigwa Jumapili, Septemba 6, 2026, katika Uwanja wa Taifa wa Bingu mjini Lilongwe, Malawi saa 12:00 jioni kwa muda wa Afrika Mashariki.

Mechi ya mkondo wa pili utafanyika nchini Tanzania Ijumaa, Septemba 11, 2026, ambapo Simba SC itakuwa wenyeji.

Mshindi wa jumla katika mechi hizo mbili atafuzu moja kwa moja kwenda hatua inayofuata ya kuwania nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.